Ansarullah: Tuko pamoja na Iran katika kukabiliana na Marekani na Israel
Harakati ya Ansarullah ya Yemen imetangaza kuwa, iko pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kukabiliana na uchokozi wa Marekani na utawala haramu wa Israel.
Hayo yameelezwa na Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen katika radiamali yake kwa hujuma za Marekani dhidi ya Iran na kusisitiza kuwa: Tunasimama pamoja na ndugu zetu wa Iran dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni.
Mohammad Al-Bakhiti, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza katika mahojiano: "Makubaliano yetu na Marekani yalikuwa ni ya kabla ya uvamizi wa nchi hii dhidi ya Iran."
Al-Bukhaiti alisema: "Leo, tunasimama pamoja na ndugu zetu nchini Iran dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni."
"Majibu yetu ya kijeshi yanakuja, na katika awamu ya kwanza, tutalenga vikosi vya Marekani katika Bahari Nyekundu," alisema.
Msimamo huo wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen umetolewa baada ya Marekani kufanya mashambulizi kwenye vito kadhaa vya nyuklia nchini Iran.