Mwanazuoni wa Ahlu‑Sunnah wa Russia: Imam Khamenei hakukubali udhalili
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i137830-mwanazuoni_wa_ahlu_sunnah_wa_russia_imam_khamenei_hakukubali_udhalili
Mufti wa Volgograd, nchini Russia amesema: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ni shahidi mkubwa wa Umma wa Kiislamu na mfuasi wa Suna ya Mtume Muhammad (S.A.W.), na jina lake litasalia katika historia kama kiongozi jasiri na mwanaume halisi.
(last modified 2026-04-12T09:00:57+00:00 )
Apr 12, 2026 08:50 UTC
  • Mwanazuoni wa Ahlu‑Sunnah wa Russia: Imam Khamenei hakukubali udhalili

Mufti wa Volgograd, nchini Russia amesema: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ni shahidi mkubwa wa Umma wa Kiislamu na mfuasi wa Suna ya Mtume Muhammad (S.A.W.), na jina lake litasalia katika historia kama kiongozi jasiri na mwanaume halisi.

Mufti Kifah Bata Hazrat hafla ya ambaye alikuwa akizungumzia kwa mnasaba wa kutimia siku arobaini baada ya kuuawa shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, amesema: "Alikuwa kama mjukuu wa Mtume Mtukufu (S.A.W.), Imam Hussein (AS) aliyechagua njia ya kufa shahadi na kukataa kudhalilishwa au kujisalimisha. Alisimama dhidi ya adui na akapata daraja tukufu ya kuuawa shahada."

Mufti wa Volgograd amesema: Mwenyezi Mungu huwapa waja wake wateule na waumini heshima ya kufa shahidi, na Kiongozi Mkuu wa Iran alipata medali hii ya tukufu.Amekumbusha kuwa: Leo Waislamu wanmadhehebu za Mashia na Masuni wa kweli wanaiombea Iran dua, kwa sababu siku 40 za vita dhidi ya Marekani na Israel hazikuwa jambo rahisi, na mapambano ya aina hii hayajawahi kurekodiwa katika historia dhidi ya maadui wa Umma wa Kiislamu.

Mwanazuoni huyo wa Kisuni wa Russia pia amepongeza mapambano na kusimama kidete watu wa Iran, Hizbullah ya Lebanon, na makundi mengine ya Muqawama katika kukabiliana na maadui, na kueleza matumaini kuwa nchi nyingine za Kiislamu pia zitajifunza kutokana na matukio ya hivi karibuni na kupiga hatua mbele katika kuimarisha udugu, upendo na umoja dhidi ya maadui wa Umma wa Kiislamu.