HAMAS: Wazayuni msidhani mtawaona tena mateka wenu
Wanamapambano wa Al-Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas, wamewahakikisha Wazayuni kwamba hawatowaona tena mateka wao hivyo wanapaswa kuwaaga kutokana na kuvamiwa Ghaza.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnimm, Brigedi za Izzuddin Al-Qassam, Tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), jana Jumamosi zilisambaza picha za mateka wa Kizayuni huko Ghaza na kutamka wazi kwamba Wazayuni hawatawaona tena mateka wao hao, hivyo lazima wawaage kabisa.
Baada ya kuchapisha picha za kuwaaga wafungwa hao, Brigedi za Al-Qassam zimesisitiza kwamba ukaidi wa Netanyahu katika kukubali usitishaji vita na uamuzi wa kushambulia Ghaza na kujisalimisha Eyal Zamir (Mkuu wa Majeshi Mkuu wa Jeshi la Israel) utawakabili (wafungwa) kwa kifo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Eyal Zamir, Mkuu wa Majeshi ya Israel, awali alipinga mpango wa Netanyahu wa kushambulia Ghaza, lakini baadaye na kwa mashinikizo ya baraza la mawaziri la Netanyahu, alikubali shambulio dhidi ya Ghaza.
Kabla ya hapo, tawi hilo la kijeshi la Hamas limeeleza katika taarifa nyingine kwamba Ghaza ni "vita vya msuguano vyenye gharama kubwa" na kuonya kwamba hatima ya mateka wa Israel inategemea harakati za kijeshi za utawala huo wa Kizayuni.
Taarifa hiyo ya Al-Qassam iliyotolewa kwa lugha ya Kiebrania ilisisitiza kuwa wanamapambano wa Hamas wamesambazwa katika vitongoji vyote vya Ghaza, wakiwa tayari kukabiliana na jeshi la utawala ghasibu wa Israel.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa, mateka wa Israel sasa wametawanywa katika vitongoji mbalimbali vya Mji wa Ghaza na kuonya kwamba vikosi vya Al-Qassam havitawahakikishia usalama wao maadamu Netanyahu angali ameazimia "kuwaua."