Utawala wa Bahrain waendeleza ukandamizaji dhidi ya raia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i16387-utawala_wa_bahrain_waendeleza_ukandamizaji_dhidi_ya_raia
Utawala wa kifalme wa Bahrain umeendelea na hatua zake za ukandamizaji dhidi ya raia wa nchi hiyo licha ya kuweko malalamiko na ukosoaji wa kimataifa dhidi ya hatua hizo ambazo zinakiuka uhuru wa raia.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Sep 30, 2016 09:34 UTC
  • Utawala wa Bahrain waendeleza ukandamizaji dhidi ya raia

Utawala wa kifalme wa Bahrain umeendelea na hatua zake za ukandamizaji dhidi ya raia wa nchi hiyo licha ya kuweko malalamiko na ukosoaji wa kimataifa dhidi ya hatua hizo ambazo zinakiuka uhuru wa raia.

Habari kutoka Manama mji mkuu wa Bahrain zinasema kuwa, raia 10 wa nchi hiyo wamehukumiwa kifungo cha miaka kumi 10 jela kwa tuhuma zisizo na msingi za kile kilichodaiwa na mahakama kuwa na uhusiano na ugaidi. Hukumu dhidi ya raia hao ilitolewa jana ambapo mbali na kuhukumiwa kwenda jela miaka kumi, raia hao wamepokonywa pia uraia.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, asasi na jumuiya mbalimbali za kutetea hakiza binadamu zimeendelea kulaani ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na utawala wa Baharain dhidi ya raia.

Ukandamizaji wa vikosi vya usalama vya Bahrain

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni nchi 35 wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa zililaani hatua zinazochukuliwa na serikali ya Bahrain dhidi ya wapinzani nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na nchi 35 wanachama wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ilielaani ukandamizaji wa serikali ya Bahrain dhidi ya wapinzani wake wa kisiasa na imetoa wito wa kufanyika marekebisho ya pande zote ya kisiasa na kurejesha utulivu nchini humo.

Tangu mwaka 2011 Bahrain imekuwa uwanja wa maandamano na wananchi dhidi ya utawala wa kifalme wa kizazi cha Aal Khalifa. Wabahrain wanataka kupewa uhuru, kuondolewa dhulma na ubaguzi na kupewa haki yao ya kimsingi ya kuchagua serikali wanayoitaka wao wenyewe badala ya kutawaliwa na kizazi cha Aal Khalifa.