Jeshi la Iraq lakomboa visima 100 vya mafuta kusini mwa Mosul
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i17713-jeshi_la_iraq_lakomboa_visima_100_vya_mafuta_kusini_mwa_mosul
Vikosi vya Iraq vimefanikiwa kukomboa visima 100 vya mafuta kusini mwa mji wa Mosul, katika operesheni maalumu ya kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa mgaidi wa Daesh.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 19, 2016 01:01 UTC
  • Jeshi la Iraq lakomboa visima 100 vya mafuta kusini mwa Mosul

Vikosi vya Iraq vimefanikiwa kukomboa visima 100 vya mafuta kusini mwa mji wa Mosul, katika operesheni maalumu ya kuukomboa mji huo kutoka mikononi mwa mgaidi wa Daesh.

Maaafisa wa mafuta nchini Iraq wametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, vikosi vya Iraq jana Jumanne viliendelea kusonga mbele na kukomboa maeneo mengi zaidi kutoka mikononi mwa magaidi wa ISIS kusini mwa Mosul, ikiwa ni pamoja na kukomboa visima 100 vya mafuta.

Maafisa wa Iraq wamesema, visima vya mafuta vya eneo la al Qayyarah lililoko umbali wa kilomita 50 kusini mwa Mosul vimekombolewa. Eneo hilo lina visima 90 vya mafuta.

Vile vile eneo la uchimbaji mafuta la Najma la kusini mwa Mosul ambalo lina visiwa 10 vya mafuta, limekombolewa kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.

Kamanda wa genge la kigaidi la Daesh akiwa ameuawa karibu na Mosul nchini Iraq

 

Maafisa hao wa Iraq wameongeza kuwa, wakati visima hivyo vilipokuwa mikononi mwa magaidi wa ISIS, mafuta yake yaliendelea kuchimbwa na mashirika ya nchi za Magharibi na kuuzwa kwa bei ya kutupa.

Mafuta ya kusini mwa Mosul ni mafuta mazito ambayo yanapendwa sana katika soko la dunia na magaidi wa Daesh walikuwa wakisafirisha kwa magendo mafuta hayo nje ya Iraq.

Maafisa wa mafuta wa Iraq wamesema, magaidi walikuwa wametega mabomu mengi ya ardhini ili kuzuia wanajeshi wa serikali wasiingie kwenye maeneo hayo, lakini vikosi vya Iraq vimefanikiwa kuingia na hivi sasa zoezi la kuvizima moto visima vilivyochomwa na magaidi wa ISIS linaendelea.