Magaidi 600 wajisalimisha kwa jeshi la Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i18025-magaidi_600_wajisalimisha_kwa_jeshi_la_syria
Magaidi 600 na watu wenye silaha wamejisalimisha kwa jeshi la Syria magharibi mwa Damascus mji mkuu wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 24, 2016 00:10 UTC
  • Magaidi 600 wajisalimisha kwa jeshi la Syria

Magaidi 600 na watu wenye silaha wamejisalimisha kwa jeshi la Syria magharibi mwa Damascus mji mkuu wa nchi hiyo.

Habari zinasema kuwa katika muda wa siku mbili magaidi na watu wenye silaha wapatao 600 wamejisalimisha kwa jeshi la Syria katika kitongoji cha al Muadhamiya magharibi mwa mji mkuu Damascus na kukabidhi silaha zao. Kwa msingi huo mgaidi hao wamestafidi pia na msamaha wa Rais wa Syria na  kurejea katika maisha yao ya kawaida.

Baadhi ya wakazi wa al Muadhamiya wakiondoka katika kitongoji hicho mwezi Septemba mwaka huu

Hadi kufikia sasa magaidi 1710 wamehamishwa kutoka katika kitongoji cha al Muadhamiya na kupelekwa katika mkoa wa Idlib kaskazini magharibi mwa Syria, kufuatia makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa kati ya jeshi la Syria na makundi ya kigaidi na yale yanayobeba silaha. Wakati huo huo serikali ya Syria imeukabidhi uongozi wa  kitongoji cha  al Muadhamiya magari 30 yaliyosheheni misaada ya chakula na vifaa vya tiba na elimu; misaada ambayo itagawiwa wakazi elfu 40 wa kitongoji hicho.