Israel haina budi kuangamiza silaha zake za nyuklia
-
Demona nuclear power plant
Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema utawala haramu wa Israel sasa hauna kisingizio cha kutotia saini Mkataba wa Kupiga Marufuku Kikamilifu Majaribio ya Silaha za Nyuklia (CTBT) baada ya mapatano ya nyuklia baina ya Iran na nchi za Magharibi.
Lassina Zerbao, katibu mtendaji wa CTBT amesema baada ya kutekekelzwa mapatano ya nyuklia ya Iran, kisingizio kikubwa zaidi cha Israel katika kukaidi takwa la kuidhinisha CTBT hakipo tena.
Ametoa kauli hiyo katika kongamano la kuadhimisha mwaka wa 20 wa kuanza kutiwa saini mkataba huo wa kuzuia majaribio ya nyuklia huko Vienna, mji mkuu wa Austria.
Mkataba wa Kupiga Marufuku Kikamilifu Majaribio ya Silaha za Nyuklia umeidhinishwa na nchi 196 lakini bado haujaanza kutekelezwa kwani unahitaji kuidhinishwa na nchi zenye silaha za nyuklia kama vile Marekani, China, India, Pakistan, Korea Kaskazini na utawala haramu wa Israel.
Inaaminka kuwa Israel inamiliki takribani vichwa vya nyuklia 200-400. Utawala huo pia umekataa kutia saini Mkataba wa Kuzuia Utegenezaji na Usambazaji Silaha za Nyuklia NPT mbali na kukaidi matakwa ya kimataifa ya kukaguliwa zana zake za nyuklia.