Russia: Marekani inafanya propaganda chafu kuhusu hospitali za Aleppo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i19807-russia_marekani_inafanya_propaganda_chafu_kuhusu_hospitali_za_aleppo
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia amesema kuwa, madai ya kushambuliwa hospitali katika mji wa Aleppo nchini Syria ni wenzo wa kipropaganda unaotumiwa na Marekani dhidi ya serikali ya Moscow.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Nov 20, 2016 00:54 UTC
  • Russia: Marekani inafanya propaganda chafu kuhusu hospitali za Aleppo

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Russia amesema kuwa, madai ya kushambuliwa hospitali katika mji wa Aleppo nchini Syria ni wenzo wa kipropaganda unaotumiwa na Marekani dhidi ya serikali ya Moscow.

Igor Konashenkov amesema kuwa, baada ya kupita siku kadhaa sasa tangu Marekani itoe madai kuwa ndege za kivita za Russia zimeshambulia hospitali na vituo vya afya katika mji wa Aleppo imebainika kuwa, picha za madai na uharibu wa hospitali hizo zinapatikana tu katika fikra za msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani John Kirby.  

Konashenkov ameongeza kuwa, madai yaliyotolewa na Marekani kuhusu kushambuliwa hospitali katika mji wa Aleppo ni urongo mkubwa unaotolewa mara kwa mara na serikali ya Washington. Amesema kuwa Moscow imekuwa ikiwataka maafisa wa serikali za Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na nchi nyingine zikiwemo jumuiya za kimataifa kutoa ripoti kuhusu vituo vya misaada ya kitiba na shule zilizoko katika maeneo yanayodhibitiwa na makundi ya kigaidi nchini Syria lakini haikupata jibu.

Magaidi wa kundi la Daesh wanaendelea kuua raia wakisaidiwa na Marekani, Saudia na washirika wao

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, John Kirby alidai Jumatano iliyopita kwamba, ndege za kivita za Russia zimeshambulia na kuharibu hospitali tano na zahanati moja katika mji wa Aleppo.