Saudi Arabia yaendelea kufanya mashambulio ya anga nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i22981-saudi_arabia_yaendelea_kufanya_mashambulio_ya_anga_nchini_yemen
Wanajeshi wa Saudi Arabia na waitifaki wao wameendelea kufanya mashambulio ya anga dhidi ya Yemen huku jamii ya kimataifa ikiendelea kunyamazia kimya jinai hizo za utawala wa Aal Saud.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 06, 2017 23:50 UTC
  • Saudi Arabia yaendelea kufanya mashambulio ya anga nchini Yemen

Wanajeshi wa Saudi Arabia na waitifaki wao wameendelea kufanya mashambulio ya anga dhidi ya Yemen huku jamii ya kimataifa ikiendelea kunyamazia kimya jinai hizo za utawala wa Aal Saud.

Ndege za kijeshi za Saudia Ijumaa ya jana kwa mara nyingine tena zilifanya mashambulio makubwa ya mabomu katika miji ya Saeda na Taiz na kusababisha uharibifu mkubwa.

Duru za habari kutoka Yemen zinasema kuwa, maeneo yaliyolengwa zaidi na mashambulio hayo ya jana ya Saudi ni Aal Sheikh katika mkoa wa Saada wa kaskazini magharibi mwa nchini hiyo na kitongoji cha al-Dhabab katika mkoa wa Taiz ambao uko kusini magharibi mwa nchi hiyo. Aidha ndege za kijeshi za Saudia ziliyashambulia kwa mabomu pia maeneo kadhaa ya mpakani ya Yemen.

Uharibifu wa Saudi nchini Yemen

Katika kujibu uchokozi huo, jeshi la Yemen na kamati za kujitolea za wananchi wa nchi hiyo zimeshambulia vituo na kambi za kijeshi za Saudia katika mji wa Jizan kusini mwa Yemen. Aidha jeshi la Yemen likishirikiana na kamati hizo za wananchi limewaangamiza mamluki kadhaa wa Saudia.

Itakumbukwa kuwa mwezi Machi mwaka 2015, kwa uungaji mkono wa Marekani, Saudi Arabia ilianzisha mashambulio dhidi ya maeneo mbalimbali ya Yemen. Moja kati ya malengo makuu ya mashambulio hayo ya kivamizi ya utawala wa Aal Saud ni kutaka kumrejesha madarakani kibaraka wake, rais aliyejiuzulu na kuitoroka nchi Abdrabbuh Mansur Hadi. Mbali kuua na kujeruhi maelfu ya raia, mashambulio ya Saudia yameteketeza pia miundombinu ya Yemen na kusababisha mamilioni ya Wayemeni kubaki bila makaazi na kuwa wakimbizi.