Wapalestina waandamana kulaani ujenzi wa vitongoji wa Israel
Wananchi wa Palestina walifanya maandamano Ijumaa ya jana kulalamikia siasa za utawala wa Kizayuni za kubomoa nyumba zao katika ardhi zilizoporwa na utawala huo mwaka 1948.
Baadhi ya wanaharakati wa Palestina akiwemo Muhammad Barakah mwakilishi wa zamani wa Knesset na ambaye pia ni mkuu wa kamati kuu inayofuatilia masuala ya Wapalestina katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 walitoa hutuba katika maandamano hayo yaliyoitishwa na kamati hiyo. Maandamano hayo yalidhuhudhriwa na maelfu ya raia wa Palestina katika makao makuu ya kijiji cha Qulansuh katika ardhi za Palestina ziliazoghusubiwa na Israel mwaka 1948.
Muhammad Barakah amesema wamiliki wa nyumba zilizobomolewa na utawala wa Kizayuni hawako peke yao na kwamba wafanya maandamano walifika katika kijiji hicho ili kuonyesha uungaji mkono wao kwa raia hao waliobomolewa nyumba zao na Israel. Mkuu wa kamati kuu inayofuatilia masuala ya Wapalestina katika ardhi zilizokaliwa kwa mabavu mwaka 19478 amesisitiza kuwa Wapalestina hawataki mapigano wala umwagaji damu, bali hawakubali nyumba zao zibomolewe. Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wanabomoa nyumba za Wapalestina kwa visingizio mbalimbali kama kutokuwa na vibali vya kujenga. Utawala wa Kizayuni mwaka jana ulizidisha hatua zake za kupora ardhi zaidi za Wapalestina ili kujenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi; kwa kadiri kwamba kiasi cha ardhi ya Wapalestina kilichoporwa na Israel mwaka jana kimeongezeka kwa asilimia 439 kulinganisha na mwaka juzi wa 2015.