Vibaraka 35 wa Saudia waangamizwa nchini Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i23806-vibaraka_35_wa_saudia_waangamizwa_nchini_yemen
Jeshi la Yemen na harakati za kujitolea za wananchi zimezuia shambulizi lililokuwa limepangwa kufanywa na vibaraka wa Saudia mjini Sana'a, mji mkuu wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 18, 2017 04:20 UTC
  • Vibaraka 35 wa Saudia waangamizwa nchini Yemen

Jeshi la Yemen na harakati za kujitolea za wananchi zimezuia shambulizi lililokuwa limepangwa kufanywa na vibaraka wa Saudia mjini Sana'a, mji mkuu wa nchi hiyo.

Katika operesheni hizo, vibaraka wasiopungua 35 wameangamizwa na wengine 68 kujeruhiwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la Yemen, makamanda wa ngazi za juu jeshini ni kati ya walioangamizwa. Hii  ni katika hali ambayo Jumatatu iliyopia jumla ya vibaraka wengine 37 wa Saudia na rais aliyejiuzulu wa Yemen, Abdurabbuh Mansour Hadi, waliangamizwa katika eneo la Usailan, lililopo mkoa wa Shabwa nchini humo.

Sehemu ya askari vibaraka wa Saudia walioangamizwa na jeshi la Yemen

Saudia ilianzisha mashambulizi yake ya kila upande ndhini Yemen hapo mwezi Machi mwaka 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani kibaraka wake, Mansour Hadi, ambapo katika hujuma hizo zaidi ya watu elfu 10 wameuawa na wengine elfu 40 kujeruhiwa. Aidha katika hujuma hizo za kikatili ndege za Saudia zimeharibu miundombinu ya kielimu, hospitali, idara za biashara, masoko na makazi ya raia.

Mmoja wa mateka wa askari vibaraka wa Saudia aliyenaswa na jeshi la Yemen

Hata hivyo hadi sasa Saudia inayoshirikiana na Marekani, Israel na mataifa ya Ulaya, imeshindwa kufikia malengo yake hayo, huku mamia ya vibaraka wake wakiangamizwa na kutekwa nyara na jeshi la Yemen.