Saudi Arabia yaendelea kuwashambulia raia wa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i23923-saudi_arabia_yaendelea_kuwashambulia_raia_wa_yemen
Ndege za kivita za Saudia zimeendelea kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya Yemen ambapo habari za hivi karibuni zinasema kuwa, ndege hizo zimefanya mashambulizi katika mikoa ya Sana'a, Taiz, Saada, Lahij na Hudaidah.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jan 20, 2017 00:54 UTC
  • Saudi Arabia yaendelea kuwashambulia raia wa Yemen

Ndege za kivita za Saudia zimeendelea kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya Yemen ambapo habari za hivi karibuni zinasema kuwa, ndege hizo zimefanya mashambulizi katika mikoa ya Sana'a, Taiz, Saada, Lahij na Hudaidah.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, ndege za Saudi Arabia zimeendelea kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo na kusababisha hasara za mali na roho za watu.

Ndege hizo zimeshambulia mara mbili barabara kuu ya Munakha katika mkoa wa Sana'a na kujeruhi raia wanne.

Ndege vamizi za Saudi Arabia zimeshambulia pia eneo la Kahbub katika mkoa wa Lahij na eneo la al Jadid la mji wa al Mukhaa katika mkoa wa Taiz huko kusini na kusini magharibi mwa Yemen.

Watoto wadogo, wanawake na raia wa kawaida ndio wahanga wakuu wa mashambulizi ya kikatili ya Saudi Arabia nchini Yemen

 

Ripoti hiyo imeongeza kuwa ndege za Saudia zimeshambulia pia eneo la Ibal la mji wa Hujailah wa mkoa wa Hudaidah, magharibi mwa Yemen.

Katika kujibu jinai hizo za Saudi Arabia, jeshi la Yemen na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu vimeshambulia kwa mizinga maeneo waliyokuwa wamekusanyika wanajeshi wa Saudia katika eneo la Najran, kusini mwa Saudia.

Wanamapambano wa Yemen aidha wameteketeza magari mawili ya mamluki wa Saudia katika mkoa wa Maarib.

Wakati huo huo Abdullah Sharif, mwandishi wa habari wa televisheni ya al Alam aliripoti jana jioni kuwa, vikosi vya ulinzi vya Yemen jana vilifanikiwa kukomboa eneo la  "Tisa" la mkoa wa Sanaa ambalo ni la milimani kutoka mikononi mwa mamluki wa Saudi Arabia.