Saudia yaendelea kuua raia wa Yemen kwa mabomu ya vishada
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i23977-saudia_yaendelea_kuua_raia_wa_yemen_kwa_mabomu_ya_vishada
Raia wengine watatu wa Yemen wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulio mapya ya anga yaliyofanywa na jeshi la Saudi Arabia katika mkoa wa Sanaá mji mkuu wa Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 21, 2017 00:48 UTC
  • Saudia yaendelea kuua raia wa Yemen kwa mabomu ya vishada

Raia wengine watatu wa Yemen wameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mashambulio mapya ya anga yaliyofanywa na jeshi la Saudi Arabia katika mkoa wa Sanaá mji mkuu wa Yemen.

Ndege za vikosi vamizi vya muungano unaoongozwa na utawala wa Aal Saud jana jioni zilishambulia eneo la tisa la mkoa wa Sanaá kwa kutumia mabomu ya vishada na kuua mwanamke mmoja mzee na watoto wadogo wawili pamoja na kuwajeruhi watoto wengine kadhaa.

Jana hiyohiyo ndege za kivita za Saudia zilishambulia karibu mara 20 eneo la makaazi ya raia la As-Sawaad katika mji mkuu wa Yemen, Sanaá na kuua na kujeruhi raia kadhaa.

Athari za mabomu ya vishada kwa watoto wa Yemen

Katika kujibu mashambulio ya Saudia, vikosi vya jeshi na vya harakati ya Ansarullah ya Yemen viemshambulia kituo cha jeshi la Saudia katika eneo la Jizan kusini mwa nchi hiyo. Shambulio hilo lililofanywa kwa kutumia mizinga na makombora liliwaangamiza na kuwajeruhi askari kadhaa wa utawaa wa Aal Saud.

Askari wengine wanne wa Saudia waliuawa hapo jana baada ya bomu kuripuka kando ya barabara yalipokuwa yakipita magari ya kijeshi ya askari hao katika kituo cha Saratih katika eneo la Jizan.../