Yemen: Hadi sasa tumeangamiza asilimia 20 ya manuwari za Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i24597-yemen_hadi_sasa_tumeangamiza_asilimia_20_ya_manuwari_za_saudia
Mkuu wa Baraza la Kisiasa nchini Yemen amesema kuwa, jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah limefanikiwa kuangamiza asilimia 20 ya manuwari za Saudi Arabia, wakati manuwari hizo zilipokuwa zikijaribu kukaribia pwani za nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 02, 2017 10:21 UTC
  • Yemen: Hadi sasa tumeangamiza asilimia 20 ya manuwari za Saudia

Mkuu wa Baraza la Kisiasa nchini Yemen amesema kuwa, jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah limefanikiwa kuangamiza asilimia 20 ya manuwari za Saudi Arabia, wakati manuwari hizo zilipokuwa zikijaribu kukaribia pwani za nchi hiyo.

Saleh Ali al-Sammad, ameongeza kuwa uelewa na irada ya wananchi wa Yemen hususan wakazi wa maeneo ya pwani ya nchi hiyo, vipelekea kufelisha njama chafu za Saudia za kutekeleza hujuma katika maeneo ya pwani ya Yemen. Al-Sammad amesisitiza kuwa, itafika siku Saudia na marafiki zake ikiwemo Marekani, Israel na mataifa mengine ya kieneno na nje ya eneo hili zitafedheheka kutokana na mashambulizi yao zinayoyafanya dhidi ya raia wa Yemen.

Sehemu ya jinai za Saudia nchini Yemen

Mwanzoni mwa wiki hii jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya Kiislamu ya Answarullah, liliiangamiza meli ndogo ya kivita ya Saudia katika maji ya pwani ya mji wa Al Hudaydah, magharibi mwa Yemen ambapo askari kadhaa wa Aal-Saud waliangamizwa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Kadhalika Saleh Ali al-Sammad, Mkuu wa Baraza la Kisiasa nchini Yemen amesema kuwa lengo la Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati ni kuibua farqa na tofauti na kwa msingi huo amewataka viongozi wa Yemen kuendeleza juhudi chanya za kisiasa kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa taifa hilo.

Mfalme wa Saudia akimvisha mkufu wa dhahabu rais wa zamani wa Marekani kama shukurani yake kwake

Saudia kwa kushirikiana na waitifaki wake, ilianzisha hujuma za kila upande dhidi ya Yemen tarehe 26 Machi mwaka 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani kibaraka wake Abdrabbuh Mansur Hadi, rais wa zamani wa Yemen ambaye alijiuzulu nafasi hiyo na kukimbilia Saudia. Hata hivyo licha ya Riyadh kufanya mauaji na uharibifu mkubwa nchini Yemen, imeshindwa kufikia malengo yake machafu nchini humo.