Jeshi la Syria lazidi kupata ushindi, lakomboa mamia ya kilomita mraba
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i24709-jeshi_la_syria_lazidi_kupata_ushindi_lakomboa_mamia_ya_kilomita_mraba
Tangu mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu hadi hivi sasa, jeshi la Syria limefanikiwa kukomboa zaidi ya maeneo 30 ya makazi ya raia kutoka kwa genge la Kizayuni na la wakufurishaji la Daesh (ISIS).
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Feb 05, 2017 01:15 UTC
  • Jeshi la Syria lazidi kupata ushindi, lakomboa mamia ya kilomita mraba

Tangu mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu hadi hivi sasa, jeshi la Syria limefanikiwa kukomboa zaidi ya maeneo 30 ya makazi ya raia kutoka kwa genge la Kizayuni na la wakufurishaji la Daesh (ISIS).

Wizara ya Ulinzi ya Russia jana Jumamosi ilitoa taarifa na kusema kuwa, katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita, jeshi la Syria limefanikiwa kukomboa makumi ya kilomita mraba za ardhi za nchi hiyo kutoka mikononi mwa Daesh.

Kituo cha kusimamia maelewano cha Russia nchini Syria nacho kimesema katika ripoti yake ya kila siku kwamba tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa, jeshi la Syria limefanikiwa kukomboa zaidi ya kilomita 1022 za ardhi ya nchi hiyo kutoka mikononi mwa magaidi wa ISIS.

Wananchi wa Syria wakisherehekea ushindi wakiwa wamenyanyua juu picha ya Rais Bashar al Assad

 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hadi hivi sasa makundi 64 yenye silaha yameshajiunga na mpango wa kuleta maelewano nchini Syria.

Wakati huo huo televisheni ya al Alam imetangtaza kuwa, jeshi la Syria na waitifaki wake, limekomboa maeneo muhimu katika viunga vya Damascus.

Habari nyingine zinasema kuwa, watoto watatu wamejeruhiwa na bomu lililokuwa limetegwa na magaidi wa Daesh katika nyumba moja kwenye kijiji cha Kufrah, katika viunga vya  Halab (Aleppo).