Iraq: Abubakar al-Baghdad amekimbilia Syria baada ya kuzidiwa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i24863-iraq_abubakar_al_baghdad_amekimbilia_syria_baada_ya_kuzidiwa
Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi amesema kuwa, kinara wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) Abubakar al-Baghdad amekimbilia nchini Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 08, 2017 04:22 UTC
  • Iraq: Abubakar al-Baghdad amekimbilia Syria baada ya kuzidiwa

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi amesema kuwa, kinara wa genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) Abubakar al-Baghdad amekimbilia nchini Syria.

Al-Abad ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Ufaransa 24 na kusema kuwa, kiongozi huyo anayesakwa kwa udi na uvumba na jeshi la Iraq amekimbilia nchini Syria kutoka Mosul yeye pamoja na wanachama wa kundi hilo wasio raia wa Iraq.

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi 

Akiashiria kuwa, magaidi hao walitoroka mji wa Mosul baada tu ya kuanza operesheni za kuukomboa mji huo, al- Abadi amesema kuwa magaidi hao waliekea Syria ili kuokoa maisha yao na kwamba sasa jeshi la Iraq linafuatilia kikamilifu nyendo za vinara wa genge hilo. Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Iraq, baada ya Abubakar al-Baghdadi kupoteza viongozi wengi wa kundi hilo katika vita na jeshi la Iraq alipatwa na wahka na kuamua kukimbia. Kadhalika amesisitiza kuwa hadi sasa gaidi huyo anayepata himaya ya kifedha na silaha kutoka Marekani, Israel na baadhi ya nchi za eneo kama vile Saudia, Qatar na kadhalika, hana tena wapiganaji wanaoweza kumlinda, kama ambavyo pia amekosa ushirikiano na makundi mengine ya kigaidi.

Abubakar al-Baghdad

Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi amesema kuwa, hivi sasa kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) linadhibiti sehemu ndogo sana ya ardhi ya Iraq yakiwemo maeneo ya Kirkuk, Nainawa (nineveh) na al-Anbar na kwamba jeshi la nchi hiyo litayadhibiti maeneo yote hayo hivi karibuni.