51 wauawa na wengine kujeruhiwa katika mlipuko wa kigaidi Baghdad
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i25226-51_wauawa_na_wengine_kujeruhiwa_katika_mlipuko_wa_kigaidi_baghdad
Gari lililokuwa limetegwa bomu limeripuka katika kitongoji kimoja kusini mwa Baghdad mji mkuu wa Iraq na kuuwa makumi ya watu na kujeruhi wengine wengi.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Feb 16, 2017 12:22 UTC
  • 51 wauawa na wengine kujeruhiwa katika mlipuko wa kigaidi Baghdad

Gari lililokuwa limetegwa bomu limeripuka katika kitongoji kimoja kusini mwa Baghdad mji mkuu wa Iraq na kuuwa makumi ya watu na kujeruhi wengine wengi.

Mlipuko huo umetokea leo wakati gari moja ambalo lilikuwa limetegwa mada mabomu liliporipuka katika mtaa mmoja wenye gereji nyingi za wauza magari huko katika wilaya ya Hayy al Shurta mjini Baghdad.

Ripoti zinasema kuwa, watu 51 wameuawa katika mlipuko huo na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Mlipuko huo wa leo umetokea siku moja baada ya ule wa jana katika kitongoji cha Sadr mjini Baghdad na kuua watu wasiopungua 15. Raia wengine 50 walijeruhiwa.

Vyombo vya habari vya Iraq vimeripoti kuwa, kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuhusika na mlipuko huo.

Magaidi wa kitakfiri wa Daesh 

Kundi la Daesh limezidisha mashambulizi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya Iraq katika kulipiza kisasi kipigo kikali kutoka jeshi la Iraq hususan katika mji wa Mosul kaskazini mwa nchi hiyo.