May 08, 2017 07:00 UTC
  • Jeshi la Israel laua shahidi binti wa Kipalestina wa miaka 16

Wanajeshi katili wa utawala haramu wa Israel wamempiga risasi na kumuua shahidi binti wa Kipalestina mashariki mwa Quds Tukufu.

Luba al-Samri, msemaji wa polisi ya utawala huo katili amesema msichana huyo wa Kipalestina ameuawa kwa kufyatuliwa risasi kwa tuhuma kuwa alitaka kuwadunga kisu maafisa wa polisi wa Israel katika Lango Kuu la Damascus, Quds Tukufu.

Hata hivyo taarifa iliyotolewa na msemaji mwingine wa polisi ya Israel, Micky Rosenfeld, imesema hakuna afisa yeyote wa polisi aliyejeruhiwa katika tukio hilo.

Mwanamke mwingine Mpalestina aliyeuawa kwa risasi na polisi ya Israel hivi karibuni

Wizara ya Afya ya Palestina imemtambulisha binti huyo kama Fatima Afif Abdu Rahman Hjeiji, mwenye umri wa miaka 16 kutoka kijiji cha Qarawat Bani Zeid, mjini Ramallah, mashariki mwa Quds Tukufu inayokaliwa kwa mabavu. 

Mbali na kuuawa shahidi binti huyo, polisi ya utawala khabithi wa Israel imemtia nguvuni mwanamke mwingine wa Kipalestina kwa jina Dunia Azmi Salhab, katika kijiji cha Tel Rumeida eneo la al-Khalil (Hebron).

Askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel kila siku wanashambulia maeneo tofauti ya Palestina na kuwaua shahidi, kuwajeruhi au kuwatia nguvuni wananchi hao madhulumu wasio na ulinzi.

Tags