Trump achochea kuzidi kukandamizwa wapinzani nchini Saudi Arabia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29690-trump_achochea_kuzidi_kukandamizwa_wapinzani_nchini_saudi_arabia
Habari kutoka nchini Saudi Arabia zinasema kuwa, ukoo wa Aal Saud unaotawala nchini humo una nia ya kutekeleza adhabu ya kifo dhidi ya mlemavu mmoja kwa tuhuma za kushiriki katika maandamano ya kuupinga utawala wa ukoo huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 28, 2017 02:24 UTC
  • Trump achochea kuzidi kukandamizwa wapinzani nchini Saudi Arabia

Habari kutoka nchini Saudi Arabia zinasema kuwa, ukoo wa Aal Saud unaotawala nchini humo una nia ya kutekeleza adhabu ya kifo dhidi ya mlemavu mmoja kwa tuhuma za kushiriki katika maandamano ya kuupinga utawala wa ukoo huo.

Gazeti la Independent la nchini Uingereza limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mahakama moja nchni Saudi Arabia imetoa hukumu ya kifo dhidi ya mtu mmoja mwenye ulemavu mwilini kwa madai ya kushiriki katika maandamano ya kupinga utawala wa nchi hiyo ingawa hakuna ushahidi wowote unaomtia hatiani mtu huyo isipokuwa maneno ya watu waliokiri chini ya mateso wakati wakisailiwa.

Licha ya uadui wake mkubwa kwa Waislamu, Donald Trump amekaribishwa kwa shangwe na furaha na viongozi wa Saudi Arabia

 

Wakati wa maandamano ya mwaka 2012, Munir Adam (23) alipigwa vibaya  sana katika eneo la Sharqiyyah, moja ya maeneo ya Waislamu wa Kishia yenye utajiri mkubwa wa mafuta nchini Saudi Arabia, na kupoteza uwezo wa kusikia sikio lake moja. Mwaka 2016 mahakama moja maalumu ya Saudia ilimuhumu kifo kwa siri mlemavu huyo.

Mkurugenzi wa taasisi moja ya kujitolea ya masuala ya sheria  amesema, rais wa Marekani Donald Trump alipotembelea Saudi Arabia hivi karibuni alishindwa kabisa kuzungumzia uvunjaji wa haki za binadamu nchini humo na jambo hilo limewapandisha kiburi viongozi wa nchi hiyo na hivi sasa wanaendelea kuwakandamiza wapinzani bila ya hofu yoyote.