Mamluki 46 wa Saudia wauawa na kujeruhiwa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i29846-mamluki_46_wa_saudia_wauawa_na_kujeruhiwa_yemen
Duru za kuaminika za Yemen zimetangaza habari ya kuuawa na kujeruhiwa karibu mamluki 46 wa Saudi Arabia katika mapigano na jeshi la Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 31, 2017 10:06 UTC
  • Mamluki 46 wa Saudia wauawa na kujeruhiwa Yemen

Duru za kuaminika za Yemen zimetangaza habari ya kuuawa na kujeruhiwa karibu mamluki 46 wa Saudi Arabia katika mapigano na jeshi la Yemen.

Televisheni ya al Alam imetangaza habari hiyo leo na kunukuu taarifa ya jeshi la Yemen ikisema kuwa, makumi ya mamluki wa Saudi Arabia wameangamizwa na kujeruhiwa katika mapigano na jeshi hilo mashariki mwa mkoa wa Taiz wa kusini magharibi mwa Yemen.

Kwa upande wao, watunga shabaha stadi wa jeshi la Yemen na wa vikosi vya kujitolea vya wananchi wamewaangamiza wanajeshi wanne wa Saudia katika mkoa wa Jizan wa kusini mwa Saudi Arabia na wanajeshi wengine waili wa Saudia katika mkoa wa Asir, wa kusini mwa nchi hiyo.

Matatizo yote yaliyoko Yemen yanatokana na uvamizi wa baadhi ya madola ya Kiarabu yanayoongozwa na Saudi Arabia

 

Vikosi vya mizinga vya jeshi la Yemen navyo vimeshambulia maeneo kijeshi ya Saudi Arabia katika mkoa wa Najran wa kusini mwa nchi hiyo.

Huko mkoani Hajjah (kaskazini magharibi mwa Yemen) pia jeshi la anga la Yemen limetungua ndege ya kijeshi ya Saudia kaskazini mwa jangwa la Midi.

Kwa upande wao, mamluki wa Saudi Arabia wameshambulia kwa maroketi makazi ya raia katika mkoa wa Taiz huko Yemen. Ndege za kivita za Saudi Arabia nazo zimefanya mashambulizi katika maeneo ya raia ya mji mkuu wa Yemen Sana'a.