Hamas yakataa wito wa Shirika la Msalaba Mwekundu
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imepinga wito uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu la kutaka kujua hatima ya askari wawili wa Kizayuni waliotoweka katika enro la Ukanda wa Gaza.
Harakati ya Hamas imesisitiza kuwa, faili la askari wa Israel wanaoshikiliwa mateka na maamuzi kuhusu askari hao yanaihusu harakati hiyo pekee na tawi lake la kijeshi.
Askari hao wawili wa Israel walitoweka baina ya mwaka 2014 na 2016 katika Ukanda wa Gaza na hatima yao haijulikani.
Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu linasisitiza kuwa, askari waliouawa vitani au kushikiliwa mateka au raia wanaoshikiliwa na adui wanapaswa kulindwa. Hata hivyo siku chache zilizopita ofisi ya shirika hilo la Msalaba Mwekundu katika Ukanda wa Gaza ilijuepusha kabisa kushughulikia mateka wa Kipalestina wanaofanya mgomo katika jela na korokoro za Israel!