Dahlan: Vitendo vya Israel Masjidul Aqswa ni ugaidi ulio wazi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i32018-dahlan_vitendo_vya_israel_masjidul_aqswa_ni_ugaidi_ulio_wazi
Mjumbe wa zamani wa Kamati Kuu ya harakati ya Fat'h ya Palestina amesema kuwa, vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji mtakatifu wa Quds na Msikiti wa al Aqsa ni ugaidi ulio wazi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 20, 2017 03:24 UTC
  • Muhammad Dahlan (kushoto) akiwa na Mahmoud Abbas, rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina
    Muhammad Dahlan (kushoto) akiwa na Mahmoud Abbas, rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina

Mjumbe wa zamani wa Kamati Kuu ya harakati ya Fat'h ya Palestina amesema kuwa, vitendo vya utawala wa Kizayuni wa Israel katika mji mtakatifu wa Quds na Msikiti wa al Aqsa ni ugaidi ulio wazi.

Muhammad Dahlan  alisema hayo jana kujibu jinai za hivi karibuni za Israel katika Msikiti wa al Aqsa na kuongeza kuwa, utawala wa Kizayuni unafanya jinai hizo kubwa huku chama cha PLO, Mamlaka ya Ndani ya Palestina na jamii ya kimataifa zikiwa zimekaa kimya kama vile hakuna jinai yoyote inayofanywa katika Kibla hicho cha kwanza cha Waislamu.

Quba jeusi la Masjidul Aqswa Palestina

 

Amesisitiza kuwa, jamii ya kimataifa leo hii inadai inapambana na ugaidi lakini inafumbia macho ugaidi unaofanywa waziwazi na Israel. Amesema, walimwengu wanapaswa kujua kuwa vijana wa Palestina wataendelea kusimama imara kukabiliana na jinai na mashambulizi ya kigaidi ya Israel.

Mjumbe huyo wa zamani wa harakati ya Fat'h huko Palestina ameongeza kuwa, wanaume, wanawake, wazee, vijana na watoto wa Palestina wanakabiliwa kwa kila namna na jinai na unyanyasaji wa utawala wa Kizayuni lakini pamoja na hayo wamesimama imara peke yao kukabiliana na njama za Wazayuni dhidi ya mji mtakatifu wa Baytul Muqaddas na Msikiti wa al Aqsa.

 

Siku ya Jumanne kundi moja la wanajeshi na walowezi wa Kizayuni waliwashambulia Waislamu wa Palestina katika eneo la nje ya msikiti huo. Makumi ya Waislamu wa Palestina walijeruhiwa katika uvamizi huo akiwemo khatibu wa Masjidul Aqswa, Sheikh Ekrima Sa'id Sabri.

Ijumaa iliyopita, utawala wa Kizayuni uliufunga Msikiti wa al Aqsa na kupiga marufuku sala bali hata adhana, baada ya wanamapambano watatu wa Palestina kufanya operesheni ya kujitolea kufa shahidi dhidi ya Wazayuni maghasibu.