Chuo Kikuu cha Queen Mary: Saudia inaeneza kipindupindu Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i33364-chuo_kikuu_cha_queen_mary_saudia_inaeneza_kipindupindu_yemen
Utafiti uliofanywa na taasisi moja ya Uingereza umebaini kuwa, muungano unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya watu wa Yemen ndio unaohusika na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen kwa kuzuia misaada ya kibinadamu na kuyazingira maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 19, 2017 23:52 UTC
  • Chuo Kikuu cha Queen Mary: Saudia inaeneza kipindupindu Yemen

Utafiti uliofanywa na taasisi moja ya Uingereza umebaini kuwa, muungano unaoongozwa na Saudi Arabia katika vita dhidi ya watu wa Yemen ndio unaohusika na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu nchini Yemen kwa kuzuia misaada ya kibinadamu na kuyazingira maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo.

Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Queen Mary cha Uingereza unasema kuwa, asilimia 78 ya kesi za ugonjwa wa kipindupindu na asilimia 81 ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo vinatokea katika maeneo yanayoshambuliwa na ndege za kivita za Saudia na washirika wake au yale yanayozingirwa na muungano huo.

Jonathan Kennedy, Andrew Harmer na David McCoy ambao ndio waliosimamia utafiti huo wanasema kuwa: Saudi Arabia na washirika wake wameharibu kabisa miundombinu ikiwa ni pamoja na hospitali na mfumo wa maji ya umma, kushambulia makazi ya raia na kuwalazimisha kukimbilia katika maeneo yasiyokuwa salama.

Wayemen wanaendelea kuaga dunia kutokana na kipindupindu

Zaidi ya watu laki tano wamekumbwa na maradhi ya kipindupindu nchini Yemen na elfu mbili miongoni mwao wameaga dunia.

Hivi karibuni tovuti ya habari cha Transcend Media Service (TMS) ilichapisha ripoti ya kutisha kuhusu mauaji ya kimbari yanayofanywa na Saudi Arabia na Marekani kwa mpangilio maalumu huko Yemen na kuandika kuwa: Ugonjwa wa kipindupindu umeenea kwa kiwango kikubwa sana nchini Yemen na vyanzo vya maji na mfumo wa majitaka wa nchi hiyo vimeharibiwa kabisa kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na ndege za kivita za Saudi Arabia. Ripoti ya Transcend Media Service (TMS) imeendelea kusema: "Hali hiyo imepeleka kuchafuka kwa maji ya matumizi ya binadamu kwa bakteria hatari wa Vibrio cholerae wanaosababisha ugonjwa wa kipindupindu ambayo sasa watumiwa na Marekani na Saudi Arabia kama silaha ya kuwaua watu wa Yemen".