Utawala wa Kizayuni wauzuia ujumbe wa bunge la Ulaya kuingia Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i34561-utawala_wa_kizayuni_wauzuia_ujumbe_wa_bunge_la_ulaya_kuingia_ghaza
Utawala wa Kizayuni umekataa kuuruhusu ujumbe wa bunge la Ulaya kulizuru eneo la Ghaza kwa lengo la kuchunguza hali mbaya ya kibinadamu iliyosababishwa katika eneo hilo na mzingiro wa kiuchumi wa utawala huo wa Kizayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 19, 2017 03:24 UTC
  • Utawala wa Kizayuni wauzuia ujumbe wa bunge la Ulaya kuingia Ghaza

Utawala wa Kizayuni umekataa kuuruhusu ujumbe wa bunge la Ulaya kulizuru eneo la Ghaza kwa lengo la kuchunguza hali mbaya ya kibinadamu iliyosababishwa katika eneo hilo na mzingiro wa kiuchumi wa utawala huo wa Kizayuni.

Neoklis Sylikiotis Mwakilishi wa bunge la Ulaya raia wa Cyprus na ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uhusiano wa Nje ya bunge hilo na Palestina jana aliwasili katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan akiongoza ujumbe wa ngazi ya juu wa wawakilishi wa bunge la Ulaya kwa ajili ya ziara ya siku nne. Katika ziara hiyo, ujumbe huo wa bunge la Ulaya utakutana na kufanya mazungumzo na maafisa, taasisi za kiraia, wanaharakati wa haki za binadamu na familia za mateka wa Kipalestina waliofungwa katika jela za utawala wa Kizayuni.  

Neoklis Sylikiotis, Mwakilishi wa bunge la Ulaya 

Hii ni katika hali ambayo utawala wa Kizayuni umeutaarifu ujumbe huo wa Umoja wa Ulaya kwamba hautaruhusiwa kufika Ghaza na kuonana na wafungwa wa Kipalestina walioko katika jela za utawala huo lengo likiwa ni kuchunguza hali ya wafungwa hao. Kundi kwa jina la " Left Integrated" katika bunge la Ulaya limelaani hatua hiyo ya Israel na kutangaza kuwa, kitendo cha kutouruhusu ujumbe wa bunge la Ulaya kufika katika eneo la Ghaza na kukutana na wafungwa wa Kipalestina ni sehemu ya siasa za Israel za kutekeleza mzingiro ulio kinyume cha sheria dhidi ya ukanda huo.