Israel: Helikopta iliyoua mwanamfalme ilishambuliwa na ndege za kivita za Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i36238-israel_helikopta_iliyoua_mwanamfalme_ilishambuliwa_na_ndege_za_kivita_za_saudia
Vyombo vya habari vya utawala haramu wa Kizayuni vimefichua kuwa, ndege za kivita za Saudi Arabia ndizo zilizohusika katika kuanguka helikopta iliyokuwa imembeba mwanamfalme wa ngazi ya juu wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 07, 2017 23:24 UTC
  • Israel: Helikopta iliyoua mwanamfalme ilishambuliwa na ndege za kivita za Saudia

Vyombo vya habari vya utawala haramu wa Kizayuni vimefichua kuwa, ndege za kivita za Saudi Arabia ndizo zilizohusika katika kuanguka helikopta iliyokuwa imembeba mwanamfalme wa ngazi ya juu wa nchi hiyo.

Helikopta iliyokuwa imembeba mwanamfalme, Mansour bin Muqrin na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Saudia ilianguka Jumapili iliyopita kusini mwa nchi hiyo ambapo watu wote waliokuwa ndani yake walifariki dunia. Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limeandika kuwa, Mansour bin Muqrin alikuwa akijaribu kutoroka Saudia kutokana na kamatakamata inayoendelea dhidi ya wanamfalme wasiokubaliana na Mohammad bin Salman bin Abdulaziz Al Saud.

Limeongeza kuwa, katika harakati zake za kujaribu kutoroka, ndege za kivita za utawala wa Aal-Saud ziliishambulia helikopta iliyokuwa imembeba na kuwaua watu wote waliokuwa ndani yake. Kabla ya hapo pia gazeti la Okaz linalochapishwa mjini Jeddah liliandika kuwa, helikopta ya Saudia iliyokuwa imembeba Mansour bin Muqrin, naibu wa gavana wa jimbo la Asir pamoja na  Saleh al-Qadhi, mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa eneo la Abha katika jimbo hilo, ilianguka katika tukio la ajali. Aidha baada ya kushuka kwa soko la hisa la Saudia katika kipindi cha saa za mwanzo wa siku ya Jumapili, makumi ya wanamfalme na baadhi ya mawaziri wa sasa na wa zamani wa nchi hiyo walitiwa mbaroni kwa tuhuma za ufisadi wa fedha.

Mgogoro wa kuwania madaraka unatokota hivi sasa Saudia

Siku ya Jumamosi utawala wa Aal-Saud uliunda kamati mpya inayoongozwa na Muhammad bin Salman kwa ajili ya kile kilichotajwa kuwa ni kupambana na ufisadi, na kuwatia nguvuni wanamfalme 11 pamoja na mawaziri 30 wa zamani na wa sasa wa nchi hiyo.