Utawala wa Kizayuni wa Israel wakiri kuwa na uhusiano na Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i36549-utawala_wa_kizayuni_wa_israel_wakiri_kuwa_na_uhusiano_na_saudia
Waziri wa Nishati wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema, Israel na Saudi Arabia zimekuwa zikiwasiliana kwa siri kuizungumzia Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 20, 2017 04:10 UTC
  • Utawala wa Kizayuni wa Israel wakiri kuwa na uhusiano na Saudia

Waziri wa Nishati wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema, Israel na Saudi Arabia zimekuwa zikiwasiliana kwa siri kuizungumzia Iran.

Yuval Steinitz ameyasema hayo katika mahojiano na redio ya jeshi la utawala wa Kizayuni na kufafanua kuwa: Israel ina uhusiano na Saudi Arabia; na Saudia inapenda uhusiano huo ubaki kuwa wa siri, lakini kwa mtazamo wa Israel hakuna tatizo lolote juu ya suala hilo.

Waziri wa Nishati wa utawala haramu wa Kizayuni amebainisha kuwa: wakati uhusiano wa Israel na Saudia au na nchi nyengine za Kiarabu unapopanuka na kustawi, Israel inaheshimu takwa la upande wa pili na kukubali kulifanya suala hilo liwe siri.

Yuval Steinitz

Hapo kabla, Waziri wa Usalama wa utawala wa Kizayuni Yisrael Katz, mbali na kutangaza kuwa Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia ametoa ombi hadharani la kumwalika Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kufanya safari ya kuitembelea Saudia, alitangaza pia kwamba mkabala na kuanzisha uhusiano wa kawaida, Tel Aviv inaweza kutoa pendekezo kwa Saudia na nchi nyengine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi la kuwa na ushirikiano wa pamoja pia wa kiusalama na kiintelijinsia.

Kushirikiana pamoja Saudi Arabia na Israel katika utekelezaji sera za kuupiga vita Muqawama na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika eneo la Mashariki ya Kati na uungaji mkono wao kwa makundi ya kigaidi vimezidi kudhihirisha na kuweka wazi sura na utambulisho halisi wa utawala wa Kizayuni na ule wa Aal Saud.../