HAMAS: Makombora yetu yataendelea kuwatwanga Wazayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i36979-hamas_makombora_yetu_yataendelea_kuwatwanga_wazayuni
Brigedi za Shahid Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimesisitiza kuwa, silaha za muqawama zitaendelea kuelekezwa upande wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 30, 2017 00:13 UTC
  • HAMAS: Makombora yetu yataendelea kuwatwanga Wazayuni

Brigedi za Shahid Izzuddin Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS zimesisitiza kuwa, silaha za muqawama zitaendelea kuelekezwa upande wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kituo cha upashaji habari ya Palestina kimezinukuu duru hizo zikisema katika tamko lake rasmi kwamba, silaha za muqawama ni nembo ya ushindi na wenzo wa kulitia nguvu taifa la Palestina katika mazungumzo na utawala wa Kizayuni, hivyo zitaendelea kuwepo.

Moussa Abu Marzouq, naibu mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas

 

Kwa upande wake, Khalil Hayyah, naibu wa mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS katika Ukanda wa Ghaza amesema kuwa, harakati hiyo inapinga hata kufanyika mazungumzo tu kuhusu silaha za muqawama, kwani silaha hizo ni kwa ajili ya kujihami taifa la Palestina mbele ya jinai za kila siku za Israel.

Msimamo huo wa Brigedi za Shahid Izzuddin Qassam umetolewa kujibu matamshi ya Hussein Sheikh na Izam Ahmad, wajumbe wawili wa kamati kuu ya harakati ya Fat'h ambao wameyataka makundi ya muqawama huko Palestina kukabidhi silaha zao kwa Mamlaka ya Ndani ya Palestina inayoongozwa na Mahmoud Abbas.

Moussa Abu Marzouq, naibu mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas pia amesema, silaha za muqawama si kitu cha kujadiliwa kabisa na kwamba umoja wa kitaifa wa Palesitna unaweza kupatikana bila ya kujiingiza katika suala la silaha za makundi ya muqawama.