Russia yatuma vikosi vya nchi kavu huko Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i3715-russia_yatuma_vikosi_vya_nchi_kavu_huko_syria
Kamanda mmoja wa ngazi ya juu wa jeshi la Russia amesema kuwa nchi hiyo imetuma huko Syria kikosi maalumu kwa ajili ya kufanya oparesheni ya upelelezi na kazi nyingine maalumu nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 24, 2016 10:37 UTC
  • Kamanda wa kikosi cha Russia
    Kamanda wa kikosi cha Russia

Kamanda mmoja wa ngazi ya juu wa jeshi la Russia amesema kuwa nchi hiyo imetuma huko Syria kikosi maalumu kwa ajili ya kufanya oparesheni ya upelelezi na kazi nyingine maalumu nchini humo.

Kanali Alexander Doring ambaye ni miongoni mwa makamanda wa kikosi cha usaidizi cha jeshi la Russia huko Syria amethibitisha kwa mara ya kwanza kuwa vikosi vya nchi kavu vya nchi hiyo vipo nchini Syria. Kanali Doring amesema kuwa hakuna haja ya kuficha ukweli wa mambo kwamba kikosi cha oparesheni maalumu cha Russia kipo nchini Syria.

Amesema wanajeshi hao wanatekeleza oparesheni ya kudhibiti na kutambua mapema harakati za magaidi kabla ya kutekelezwa mashambulizi ya anga. Ameongeza kuwa kikosi hicho pia kinaongoza ndege kulenga maeneo ya mbali na shughuli nyingine.