Dakta Velayati: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijaipatia kombora Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i37741-dakta_velayati_jamhuri_ya_kiislamu_ya_iran_haijaipatia_kombora_yemen
Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu haijaipatia kombora lolote Yemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 18, 2017 01:12 UTC
  • Dakta Velayati: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijaipatia kombora Yemen

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu haijaipatia kombora lolote Yemen.

Dakta Ali Akbar Velayati ametoa majibu kwa madai ya Nikki Haley, balozi na mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa na kusema kuwa, mtu huyu kwa akali hana ufahamu wa kutosha wa kuzungumza na anazungumza mambo yasiyo na msingi wowote.

Mshauri wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika masuala ya kimataifa amesisitiza kuwa, si kweli kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeipatia kombora Yemen na madai haya hayana msingi wowote ule.

Nikki Haley, mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa

Niki Haley balozi na mwakilishi wa kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alidai siku ya Alkhamisi  kuwa, mabaki ya makombora ya Iran yamepatikana katika ardhi ya Saudia, madai yasiyo na msingi ambayo yamepingwa haraka sana  hata na Umoja wa Mataifa wenyewe.

Kuhusiana na hatua ya Rais Donald Trump ya kutangazaa Beitul-Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel, Dakta Ali Akbar Velayati amesisitiza kuwa, hapana shaka yoyote kwamba, Beitul-Muqaddas yote ni mji mkuu wa Palestina.

Katika upande mwingine, Velayati ameashiria matunda ya makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kubainisha kwamba, Marekani imekuwa ikifanya kila iwezalo ili kufanya mambo kinyume na makubaliano haya ya kimataifa.