Hamas: Wapalestina hawaogopi vitisho vya utawala haramu wa Israel
(last modified Tue, 20 Feb 2018 04:02:28 GMT )
Feb 20, 2018 04:02 UTC
  • Hamas: Wapalestina hawaogopi vitisho vya utawala haramu wa Israel

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, wananchi wa Palestina hawaogopeshwi na vitisho vya utawala dhalimu wa Israel.

Hazim Qassim amesema katika radiamali yake kwa matamshi ya jana ya Yoav Mordechai, mratibu wa Wazayuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina kwamba, wananchi wa Ukanda wa Gaza katu hawatishiki na vitisho vya viongozi wa utawala ghasibu wa Israel.

Yoav Mordechai alidai jana kwamba, jeshi la Israel litachukua hatua dhidi ya Wapalestina wanaoandamana katika mpaka wa Ukanda wa Gaza na ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na ambazo ndizo zinazojulikana kama Israel.

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, kile kinachofuatiliwa na utawala ghasibu wa Israel ni kuhalalisha mauaji dhidi ya waandamanaji wa Kipalestina.

Rais Donald Trump wa Marekani

Tangu Disemba 6 mwaka jana maeneo mbalimbali ya Palestina na Ukanda wa Gaza yamekuwa yakishuhudia maandamano makubwa dhidi ya Rais Donald Trump wa Marekani baada ya kiongozi huyo kuitangaza Beitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala haramu wa Israel na kuitaka Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya nchi hiyo kuanza mchakato wa kuuhamisha ubalozi wa Washington kutoka Tel Aviv na kuupeleka huko Beitul-Muqaddas.

Uamuzi huo wa Rais wa Marekani umeendelea kulaaniwa katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu na yasiyo ya ulimwengu wa Kiislamu.

Tags