Israel yaanza tena kujenga ukuta wa kibaguzi katika mpaka wa Lebanon
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i42846-israel_yaanza_tena_kujenga_ukuta_wa_kibaguzi_katika_mpaka_wa_lebanon
Utawala wa Kizayuni jana Jumapili ulianza tena kujenga ukuta wake wa kibaguzi kati ya mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Lebanon.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 09, 2018 02:27 UTC
  • Israel yaanza tena kujenga ukuta wa kibaguzi katika mpaka wa Lebanon

Utawala wa Kizayuni jana Jumapili ulianza tena kujenga ukuta wake wa kibaguzi kati ya mpaka wa Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Lebanon.

Ukuta huo wa zege umeanza kujengwa tena mkabala na vitongoji viwili vilivyoko mpakani vya Kafrikala na al Adisa huko kusini mwa Lebanon katika hali ambayo ujenzi wa ukuta huo ulisimamishwa mwishoni mwa mwezi Februari iliyopita baada ya ndege ya kivita ya jeshi la Syria kuitungua ndege ya kivita ya Israel aina ya F-16. 

Viongozi wa Lebanon ambao wanaitambua hatua hiyo ya kuanza tena kujengwa ukuta huo wa kibaguzi wa Israel kuwa ni uvamizi dhidi ya ardhi nzima ya nchi hiyo wamesema kuwa yapo masuala 13 kuhusu mpaka yenye kuzua hitilafu kati ya Lebanon na Israel;  ambapo hadi kufikia sasa hakuna maeneo ya mipaka ya kimataifa iliyoainishwa kati ya pande mbili hizo.  

Yaacoub Sarraf, Waziri wa Ulinzi wa Lebanon huko nyuma aliwahi kuitahadharisha jamii ya kimataifa kuhusu kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuitaka ichukue hatua za kuzuia mashambulizi hayo ya utawala huo ghasibu.

Yaacoub Sarraf, Waziri wa Ulinzi wa Lebanon 

Wakati huo huo Gadi Eizenkot, Mkuu wa majeshi ya utawala wa Kizayuni tarehe Pili mwezi huu alidai kuwa Israel imeainisha maelfu ya maeneo huko Lebanon ambayo  iwapo kutatokea vita kati yake na harakati ya Hizbullah utawala huo haramu utatoa pigo kwa maeneo hayo.