Balozi wa Palestina UN ataka kuchunguzwa jinai za Israel huko Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i43414-balozi_wa_palestina_un_ataka_kuchunguzwa_jinai_za_israel_huko_gaza
Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa umoja huo kuunda kamisheni huru ya kuchunguza jinai za kutisha zinazofanywa na wanajeshi katili wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 20, 2018 23:40 UTC
  • Balozi wa Palestina UN ataka kuchunguzwa jinai za Israel huko Gaza

Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa umoja huo kuunda kamisheni huru ya kuchunguza jinai za kutisha zinazofanywa na wanajeshi katili wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Riyad Mansour aliyasema hayo jana Ijumaa katika kikao na waandishi wa habari mjini New York, saa chache baada ya wanajeshi hao wa Kizayuni kuua shahidi Wapalestina wengine wanne, waliokuwa wakishiriki maandamano ya amani katika mpaka wa Gaza.

Amesema anatumai kuwa Umoja wa Mataifa utapasisha azimio la kuanzishwa uchunguzi huru na wa wazi wa jinai hizo za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina, kama alivyopendekeza Katibu Mkuu wa umoja huo, Antonio Guterres.

Kadhalika mjumbe huyo wa Palestina katika UN amesisitiza kuwa, lazima watenda jinai wote wa Israel wakabiliwe na mkono wa sheria kutokana na ukatili walioufanya dhidi ya Wapalestina, huku akiishangaa jamii ya kimataifa kwa kufumbia macho jinai hizo za kutisha.

Waandamanaji wa Kipalestina wakiubeba mwili wa mmoja wa mashahidi

Hapo jana Wapalestina wanne waliokuwa wakishiriki maandamano ya amani katika Ukanda wa Gaza waliuawa shahidi kwa risasi za utawala ghasibu wa Israel, huku wengine zaidi ya 40 wakijeruhiwa, na hivyo kupelekea idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi kufikia sasa kupindukia 35, ndani ya wiki tatu.

Maandamano ya amani ya 'Haki ya Kurejea' yaliyoitishwa na Wapalestina kwa ajili ya kupigania haki ya kurejea wakimbizi wa taifa hilo katika ardhi zao walizoporwa na Wazayuni mwaka 1948 yalianza Machi 30, na yanatazamiwa kuendelea hadi Mei 15.