Hamas: Utawala wa Kizayuni ndio uliomuuwa Fadi al Batsh
(last modified Fri, 27 Apr 2018 07:49:28 GMT )
Apr 27, 2018 07:49 UTC
  • Hamas: Utawala wa Kizayuni ndio uliomuuwa Fadi al Batsh

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeutaja utawala wa kizayuni wa Israel kuwa ndio uliomuua Fadi al Batsh msomi na mwanasayansi wa Kipalestina huko Malaysia.

Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas Khalil al Hayyah amesema katika shughuli ya kupokea mwili wa msomi wa Kipalestina, Fadi al Batsh katika kivuko cha mpakani cha Rafah kuwa utawala wa Kizayuni ndio uliomuua mhandishi huyo wa Kipalestina. 

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa mwendazake Fadi al Batsh huko Ghaza

Mjumbe huyo wa ngazi ya juu wa Ofisi ya Kisiasa ya Hamas amesisitiza kuwa jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel itajibiwa.

Familia ya al Batsh pia imesema kuwa Shirika la Ujasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel (Mossad) ndilo lilitekeleza jinai hiyo. Vilevile gazeti la New York Times la Marekani limeripoti kuwa mauaji ya msomi huyo wa Palestina huko Malaysia yamefanyika kwa usimamizi na mwongozo wa shirika la ujasusi la Isarel, MOSSAD.

Fadi al Batsh aliuawa Jumamosi iliyopita na watu wasiojulikana huko Kuala Lumpur nchini Malaysia. Mwili wa marehemu al Batsh jana alasiri uliwasili Ukanda wa Ghaza kupitia kivuko cha mpakani cha Rafah. Makumi ya raia wa Palestina, viongozi na makundi ya Kipalestina yalishiriki katika marasimu hayo ya kuupokea mwili wa msomi huyo. 

Tags