Wapiganaji wa Hashdu sh-Sha'abi wawaangamiza magaidi wa Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i43874-wapiganaji_wa_hashdu_sh_sha'abi_wawaangamiza_magaidi_wa_daesh
Duru kutoka Iraq zimearifu kuwa wapiganaji wa harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi wamewaua magaidi kadhaa wa kundi la kitakfiri la Daesh katika mashambulizi waliyofanya katika eneo moja katika mpaka wa Iraq na Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 30, 2018 23:42 UTC
  • Wapiganaji wa Hashdu sh-Sha'abi wawaangamiza magaidi wa Daesh

Duru kutoka Iraq zimearifu kuwa wapiganaji wa harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Sha'abi wamewaua magaidi kadhaa wa kundi la kitakfiri la Daesh katika mashambulizi waliyofanya katika eneo moja katika mpaka wa Iraq na Syria.

Duru hizo za habari zimearifu kuwa kikosi cha 27 cha wapiganaji wa Hashdu sh-Sha'abi wa Iraq huku wakisaidiwa na kikosi cha vifaru jana walitekeleza shambulizi katika eneo la al Sayba walipokuwa magaidi hao wa Daesh katika mpaka wa Iraq na Syria.   

Habari nyingine zinasema kuwa wanawake 6 wanachama wa kundi hilo ambao ni raia wa Azerbaijan wamehukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela huko Iraq. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mbali na wanawake hao sita wanachama wa Daesh ambao ni raia wa Azerbaijan, raia wengine 19 wa Russia na wanne kutoka Tajikistan pia wamehukumiwa kifungo cha maisha jela na mahakama ya Baghdad.

Wanachama wa Daesh kutoka mataifa mbalimbali 

Siku kadhaa zilizopita mkuu wa kamati ya kiserikali inayohusika na masuala ya makundi ya kidini, mkuu wa idara ya usalama wa serikali na Waziri wa Mambo ya Nje wa Azerbaijan waliripotiwa kufanya mazungumzo na serikali ya Iraq sambamba na serikali ya Baku kufanya juhudi za kuwarejesha nchini wanawake hao wa Kidaesh na raia wengine wa Azerbaijan ambao walijiunga na kundi hilo la kitakfiri na kwamba kuna uwezekano raia hao waliuawa huko Iraq.