Russia yalalamikia jinsi Marekani inavyopigania kuwarejesha magaidi wa ISIS nchini Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i45640-russia_yalalamikia_jinsi_marekani_inavyopigania_kuwarejesha_magaidi_wa_isis_nchini_syria
Wizara ya Ulinzi ya Russia imefichua kuwa, Marekani inafanya juhudi kubwa za kuwarejesha magaidi wa Daesh (ISIS) nchini Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 09, 2018 22:20 UTC
  • Russia yalalamikia jinsi Marekani inavyopigania kuwarejesha magaidi wa ISIS nchini Syria

Wizara ya Ulinzi ya Russia imefichua kuwa, Marekani inafanya juhudi kubwa za kuwarejesha magaidi wa Daesh (ISIS) nchini Syria.

Hayo yametangazwa na televisheni ya Rusia al Yaum ambayo imeinukuu wizara ya ulinzi ya Russia ikisema kuwa, hivi sasa magaidi wa Daesh wamebakia tu katika maeneo ambayo yanadhibitiwa na wanajeshi wa Marekani huko Syria.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Russia vile vile amesema, mchakato wa kuimarisha utulivu na amani umezaa matunda mazuri na unaendelea vyema katika maeneo yaliyokombolewa na serikali ya Syria na hivi sasa operesheni za kutegua mabomu ya kutegwa ardhini zinaendelea. Aidha amesema, tayari taasisi mbalimbali, masoko, shule, chekechea na mabustani ya maeneo hayo yamesharejea katika hali zake za kawaida kama ilivyokuwa kabla ya Syria kuvamiwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na vibaraka wao, mwezi Machi 2011.

Wanajeshi wa Marekani nchini Syria

 

Msemaji huyo wa wizara ya ulinzi ya Russia ameongeza kuwa, misaada ya kibinadamu na chakula kinasambazwa vizuri katika maeneo yaliyokombolewa na serikali ya Syria, lakini Marekani haijatenga chochote katika bajeti yake kwa ajili ya kuwasaidia wakazi wa maeneo ambayo yako mikononi mwake huko Syria.

Mara kwa mara serikali ya Damascus imekuwa ikilaani kuwepo kijeshi Marekani nchini Syria na imekuwa ikisisitiza kuwa huo ni uvamizi na ni kutoheshimu haki ya kujitawala nchi hiyo.