Mjumbe wa UN kuitembelea Tehran kuhusu mgogoro wa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i4642-mjumbe_wa_un_kuitembelea_tehran_kuhusu_mgogoro_wa_syria
Staffan de Mistura mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria anatazamiwa kuitembelea Iran karibuni hivi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 08, 2016 03:47 UTC
  • Mjumbe wa UN kuitembelea Tehran kuhusu mgogoro wa Syria

Staffan de Mistura mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria anatazamiwa kuitembelea Iran karibuni hivi.

Katika kikao na waandishi wa habari jana, Mistrura alisema anapanga kuitembelea Tehran na Damascus kati kati ya mwezi huu. Awali Mjumbe huo wa UN aliashiria kuwa huenda akaja nchini kabla ya kuanza duru mpya ya mazugumzo ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Syria.

Aidha Staffan de Mistura mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Syria anatazamiwa kuzitembelea Uturuki, Saudi Arabia, Jordan na Lebanon kabla ya kikao hicho.

Awali de Mistura aliaashiria kuwa huenda duru mpya ya mazungumzo ya Syria ikaanza kati ya Aprili 9 na 11.

Haya yanajiri katika hali ambayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry, ameomba msaada wa Iran ili kuhatimisha vita katika nchi za Syria na Yemen. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani aliyasema hayo mbele ya waandishi wa habari mapema jana kabla ya mazungumzo yake na mawaziri wenzake wa nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi huko nchini Bahrain.

Serikali ya Syria inasema nchi za Magharibi na waitifaki wao katika eneo la Mashariki ya Kati hasa Utawala haramu wa Israel, Saudi Arabia, Qatar na Uturuki ndio waungaji mkono wakuu wa magaidi wanaotaka kuiangusha serikali ya Rais Bashar al-Assad.