Muqtada Sadr ataka kusimamishwa mazungumzo ya kuundwa serikali mpya ya Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i46893-muqtada_sadr_ataka_kusimamishwa_mazungumzo_ya_kuundwa_serikali_mpya_ya_iraq
Moqtada al-Sadr, kiongozi wa muungano wa Sairun, nchini Iraq ametaka kusimamishwa mazungumzo yenye lengo la kuundwa serikali mpya, hadi pale kutakapotekelezwa matakwa ya walalamikaji.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 20, 2018 02:58 UTC
  • Muqtada Sadr ataka kusimamishwa mazungumzo ya kuundwa serikali mpya ya Iraq

Moqtada al-Sadr, kiongozi wa muungano wa Sairun, nchini Iraq ametaka kusimamishwa mazungumzo yenye lengo la kuundwa serikali mpya, hadi pale kutakapotekelezwa matakwa ya walalamikaji.

Katika hali ambayo maandamano ya wakazi wa kusini mwa Iraq yamekuwa yakiendelea kwa muda wa siku 10 sasa sambamba na serikali ya nchi hiyo kutekeleza hatua na kauli kadhaa, Moqtada al-Sadr ametoa kauli ya kusimamishwa mwenendo wa mazungumzo yenye lengo la kuundwa serikali hadi pale kutakapoundwa idara za utatuzi wa mgogoro kati ya serikali na waandamanaji hao. Mwanazuoni huyo ameyasema hayo kupitia ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.

Maandamano ya Wairaqi

Moqtada al-SadrAidha katika uwanja huo, ameyataka makundi ya kisiasa yaliyoshinda katika uchaguzi, kusimamisha pia mazungumzo yao juu ya namna ya kuundwa bunge na masuala mengine yanayohusiana na kadhia hiyo. Hii ni katika hali amabayo, Jumatano usiku Fuad Masum, Rais wa Iraq katika mkutano wake na makundi ya kisiasa nchini humo, sambamba na kauashiria maandamano ya hivi karibuni kusini mwa nchi, alisema kuwa, kwa kuzingatia matukio hayo kuna udharura wa kuundwa haraka serikali. Maandamano ya hivi karibuni nchini Iraq yalianzia mjini Basra, kusini mwa nchi katika kulalamikia kupungua kwa umeme, maji na ukosefu wa ajira kwa vijana na kuenea pia katika maeneo mengine ya nchi.