UN yatoa mapendekezo ya kuboresha hali ya Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i47527-un_yatoa_mapendekezo_ya_kuboresha_hali_ya_wapalestina
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mapendekezo kadhaa ya kuwasaidia watu wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 18, 2018 10:00 UTC
  • UN yatoa mapendekezo ya kuboresha hali ya Wapalestina

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mapendekezo kadhaa ya kuwasaidia watu wa Palestina katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.

Katika ripoti yake yenye kurasa 14 ambayo imetayarishwa kwa takwa la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema kuwa utekelezaji wa mapendekezo hayo unategemea ushirikiano wa utawala wa Israel na watu wa Palestina, lakini inaonekana kuwa Israel huenda isiafiki mpango huo. 

Mpango wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa unajumuisha suala la kuimarishwa uwepo wa UN katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu, kuzidishwa misaada ya kibinadamu kwa ajili ya koboresha hali ya Wapalestina, kuundwa kamati ya kiraia ya kusimamia maeneo muhimu kama vituo vya upekuzi na kupelekwa kikosi cha UN katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.

Hata watoto wadogo wa Palestina wanauawa kinyama kwa kupigwa risasi.. 

Mapendekezo hayo ya Antonio Guterres yanahitaji kupasishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili yaweze kutekelezwa. Kwa msingi huo inatabiriwa kuwa, kwa vile mapendekezo hayo yanawanufaisha watu wa Palestina, Marekani itatumia kura ya veto kukwamisha utekelezaji wake. 

Mapendekezo hayo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yametolewa baada ya Wapalestina 171 kuuawa kwa kupigwa reisasi na askari wa Israel kuanzia mwezi Machi mwaka huu wakiwa katika maandamano ya amani yaliyopewa jina la Haki ya Kurejea.