Wanajeshi wa Israel wameua watoto 54 Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i50293-wanajeshi_wa_israel_wameua_watoto_54_wapalestina
Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wameua watoto 54 Wapalestina katika mwaka huu wa 2018 unaomalizika.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Dec 20, 2018 01:13 UTC
  • Wanajeshi wa Israel wameua watoto 54 Wapalestina

Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wameua watoto 54 Wapalestina katika mwaka huu wa 2018 unaomalizika.

Kwa mujibu wa Kituo cha Haki za Binadamu cha Palestina, asilimia 80 ya watoto hao waliuawa katika maandamano ya amani ya Wapalestina katika mpaka wa Ukanda wa Ghaza na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, Jeshi la Israel  limewakamata watoto wengine 900 tokea Januari mwaka huu. Ripoti hiyo imesema kuwa wanajeshi wa Israel hukiuka haki za watoto hao waliokamatwa ambao huteshwa vibaya.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2018, Wapalestina  zaidi ya 310 wameuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel na aghalabu ya waliouawa walikuwa ni raia ambao hawakuwa na silaha.

Mazishi ya watoto waliouawa shahidi na wanajeshi wa Israel 

Mwezi Okotoba, Harakati ya Kupigania Ukombozi wa Palestina, PLO, ilisema jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limekuwa likiwaua kwa makusudi watoto wa Palestina. Mwanachama wa Kamati ya Utendaji ya PLO, Bi. Hannan Ashrawi anasema vitendo hivyo vya Israel ni ukiukwaji wa wazi wa sheria na kanuni za   kimataifa.