Kikao cha OIC Istanbul na mifarakano inayozushwa na Saudia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i5032-kikao_cha_oic_istanbul_na_mifarakano_inayozushwa_na_saudia
Kikao cha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC wanakutana leo Alkhamisi na kesho Ijumaa katika mji wa Istanbul nchini Uturuki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 14, 2016 07:56 UTC
  • Kikao cha OIC Istanbul na mifarakano inayozushwa na Saudia

Kikao cha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC wanakutana leo Alkhamisi na kesho Ijumaa katika mji wa Istanbul nchini Uturuki.

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kati ya viongozi wanaoshiriki katika kikao hicho ambacho kimetanguliwa na kikao cha mawaziri wa mambo ya nje wanachama wa OIC.

Akihutubia kikao hicho cha mawaziri, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alisisitiza kuhusu udharura wa kuimarishwa umoja miongoni mwa nchi za Kiislamu. Zarif pia ametoa jibu kwa uchochezi wa Saudia dhidi ya Iran. Ameashiria hatua ya Saudia kuwasilisha maudhui iliyo dhidi ya Iran na Harakati ya Hizbullah ya Lebanon katika rasimu ya taarifa ya mwisho ya OIC na kusema hatua hiyo ni kinyume cha moyo wa mshikamano wa Kiislamu na ni kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni.

Zarif ameonya kuhusu matokeo mabaya ya mueleleko huo haribifu na kusema, mbinu ya Saudia inashabihiana na ile iliyotumiwa na utawala ulioangushwa wa Saddam Hussein huko Iraq ambaye alikuwa akitumia vibaya OIC wakati wa vita vya kulazimishwa vya nchi hiyo dhidi ya Iran.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amehoji ni kwa nini baadhi ya nchi wanachaam wa OIC zinafuatilia sera hizo za Saddam zilizofeli.

Hakuna shaka kuwa kuendelea sera hasi na za kuibua mifarakano za Saudia katika eneo ni kwa madhara ya wote.

Saudia inapeleka uhasama katika kikao cha OIC huko Istanbul katika hali ambayo kikao hicho kinapaswa kuwa ni fursa ya Iran na nchi zote za Kiislamu kuweza kuwasilisha taswira nzuri ya Uislamu duniani.

Masuala ya Palestina, Syria, Yemen, Libya na hali mbaya ya Waislamu barani Afrika, tishio la Israel na Daesh ni kati ya maudhui zinazojadiliwa katika kikao hicho cha OIC na maamuzi muhimu kuchukuliwa.

Tunapaswa kukubali kuwa, malumbano na kuchafuliana jina nchi za Waislamu ni jambo ambalo litadhoofisha hadhi ya Uislamu duniani na jambo hilo litakuwa kwa manufaa ya maadui wa Uislamu hasa utawala haramu wa Israel.

Nukta hii ni muhimu haswa kwa kuzingatia kuwa matatizo mengi ya ulimwengu wa Kiislamu yanachochewa na nchi za kigeni kupitia sera za uingiliaji na uibuaji mgogoro wa madola ya kibeberu ambayo yanataka kuzitwisha nchi za Kiislamu sera zao za kisiasa na kiuchumi ili ziendelee kubakia nyuma katika sekta zote za ustawi.

Nchi za Kiislamu zinashambuliwa kidhulma na vyombo vya habari vya Magharibi ambavyo vinaeneza chuki dhidi ya Uislamu. Hali kadhalika Waislamu ni waathirika wakuu wa ugaidi ambao nchi za Magharibi zimeuelekeza kwa nchi za Kiislamu.

Inatazamiwa kuwa, ujumbe wa kikao cha Istanbul kwa waliwmengu utakuwa ujumbe wa umoja na mashikamano wa ulimwengu wa Kiislamu na utautzi wa migogoro ya nchi za Kiislamu.

Lakini sera za Saudia ni kinyume na maslahi ya nchi za Kiislamu na pia kudhoofisha mrengo wa mapambano dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Katika upande wa pili, nchi za Magharibi nazo zinaendeleza njama za kuibua mifarakano katika nchi za Kiislamu duniani. Marekani na waitifaki wake wamejikita katika kuibua hofu dhidi ya Iran katika eneo. Kutolewa ripoti mpya ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani kuhusu kile kinachodaiwa ni ukiukwaji wa haki za binadamu Iran, kuongezwa muda wa vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Iran kwa kisingizio hichohicho sambamba na uchochezi wa Saudia dhidi ya Iran ni mambo yaliyofanyika katika fremu ya kueneza chuki dhidi ya Iran. Nukta hii inaonyesha kuwa nchi za Magharibi na waitifaki wao katika eneo wanataka kuzuia umoja wa nchi za Kiislamu. Wamepanga njama ya kuhakikisha kuwa kikao cha OIC mjini Istanbula kinageuka na kuwa uwanja wa malumbano ya nchi za Kiislamu. Kwa msingi huo uchochezi wa Saudia katika kikao hicho ni huduma ya wazi kwa maslahi ya maadui wa umma wa Kiislamu.