Jeshi la Israel limeua shahidi Wapalestina 11 mwezi mmoja uliopita
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i51270-jeshi_la_israel_limeua_shahidi_wapalestina_11_mwezi_mmoja_uliopita
Jeshi la Utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi Wapalestina 11 katika mwezi uliopita wa Januari.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 01, 2019 23:17 UTC
  • Jeshi la Israel limeua shahidi Wapalestina 11 mwezi mmoja uliopita

Jeshi la Utawala wa Kizayuni wa Israel limewaua shahidi Wapalestina 11 katika mwezi uliopita wa Januari.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Quds Press,tokea mwanzo wa mwezi Januari 2019, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewaua shahidi Wapalestina watano katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na wengine 6 katika Ukanda wa Ghaza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo,  Wapalestina wengine 1,200 wamejeruhiwa baada ya kuhujumiwa na askari wa utawala haramu wa Israel na walowezi wa Kizayuni.

Aidha katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita Wazayuni wamebomoa, majengo 35 ya Wapalestina zikiwemo nyumba 10 za makazi huku nyumba zingine 30 zikipewa notisi ya kubomolewa.

Mpalestina akiomboleza mwenzake aliyeuawa shahidi na wanajeshi katili wa Israel

Hali kadhalika utawala wa Kizayuni wa Israel unashikilia miili 38 ya mashahidi Wapalestina. 

Kwa ujumla, Jeshi la utawala haramu wa Israel limeua zaidi ya Wapalestina 254 na kuwajeruhi wengine wasiopungua 23,000 tokea yaanze 'Maandamano Makubwa ya Haki ya Kurejea' ambayo yamekuwa yakifanyika kila Ijumaa kuanzia Machi 30 mwaka 2018.