Haniyeh: Israel inakabiliwa na mazingira magumu sana ya baadaye
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i52360-haniyeh_israel_inakabiliwa_na_mazingira_magumu_sana_ya_baadaye
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniyeh amesema kuwa, utawala haramu wa Israel unatakiwa kufahamu ujumbe wa maandamano ya kurejea yanayoendelea katika mpaka wa Ukanda wa Ghaza na ardhi nyingine za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel na kwamba kinyume na hivyo basi utakabiliwa na mustakbali mgumu zaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 23, 2019 21:58 UTC
  • Haniyeh: Israel inakabiliwa na mazingira magumu sana ya baadaye

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS, Ismail Haniyeh amesema kuwa, utawala haramu wa Israel unatakiwa kufahamu ujumbe wa maandamano ya kurejea yanayoendelea katika mpaka wa Ukanda wa Ghaza na ardhi nyingine za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel na kwamba kinyume na hivyo basi utakabiliwa na mustakbali mgumu zaidi.

Akielezea maandamano ya wiki hii ya Haki ya Kurejea sambamba na kubainisha kwamba maandamano hayo yataendelea hadi pale yatakapofikia malengo yake, amesema kuwa, kamwe Wapalestina hawatorejea nyuma. Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS sambamba na kusisitiza kwamba maandamano hayo yamethibitisha uimara wa raia wa Palestina katika kudai haki yao, amefafanua kwamba Wapalestina wameshikamana vilivyo kwa ajili ya kuzuia utekelezwaji wa mpango wa Marekani na Israel wa 'Muamala wa Karne.'

Ismail Haniyeh, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS

Amezidi kubainisha kwamba Muqawama wa Palestina unafuatilia kwa karibu hali ya kibinaadamu ya Wapalestina na ni kwa ajili hiyo ndio maana harakati hiyo pamoja na makundi mengine ya muqawama yanalipa kipaumbele suala la kuvunjwa mzingiro na kuhitimisha mateso ya Wapalestina. Maandamano ya haki ya kurejea yalifanyika jana Ijumaa ambapo pia imepangwa kufanyika maandamano makubwa kama hayo hapo tarehe 30 ya mwezi huu kwa mnasaba wa kutimia mwaka mmoja tangu vuguvugu hilo lilipoanzishwa tarehe kama hiyo mwaka jana.