Hizbullah: Lengo letu ni kuuangamiza utawala wa kizayuni wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i52970-hizbullah_lengo_letu_ni_kuuangamiza_utawala_wa_kizayuni_wa_israel
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, njia ya harakati hiyo ni kufuata maktaba ya Uislamu na kuuangamiza utawala ghasibu wa Israel unaoikalia kwa mabavu Beituul-Muqaddas.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 20, 2019 03:37 UTC
  • Hizbullah: Lengo letu ni kuuangamiza utawala wa kizayuni wa Israel

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, njia ya harakati hiyo ni kufuata maktaba ya Uislamu na kuuangamiza utawala ghasibu wa Israel unaoikalia kwa mabavu Beituul-Muqaddas.

Sheikh Naim Qassim amesema hayo mjini Beirut Lebanon katika mazungumzo yake na ujumbe wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kueleza kuwa, uhusiano wa Hizbullah na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni katika neema za Mwenyezi Mungu.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon  amebainisha kuwa, misaada ya Iran hususan ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH kumeilea Hizbullah na kuipa nguvu na kuwafanya wapiganaji wa harakati hiyo wapate ushindi katika vita vyao na adui Mzayuni.

Wapiganaji wa Hizbullah ya Lebanon

Amir Khojasteh, mkuu wa ujumbe wa Bunge la Iran naye amepongeza na kusifu mchango wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon katika kuunda mhimili wa muqawama na mapambano katika miaka ya hivi karibuni.

Katika kipindi cha siku mbili cha kuwa kwake Beirut, ujumbe wa Bunge la Iran unatarajiwa kukutana na baadhi ya viongozi wa makundi ya mapambano ya Kiislamu ya Palestina  akiwemo Saleh al-Arouri, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS na Ziyad al-Nakhalah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina.