Ubalozi wa Palestina Tehran: Trump ni kijakazi cha Netanyahu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i53359-ubalozi_wa_palestina_tehran_trump_ni_kijakazi_cha_netanyahu
Ubalozi wa Palestina katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kukosoa vikali sera za Rais Donald Trump wa Marekani za kuunga mkono na kuukingia kifua utawala wa Kizayuni wa Israel, umebainisha kuwa Trump anapokea na kutekeleza maagizo kutoka kwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 08, 2019 23:46 UTC
  • Ubalozi wa Palestina Tehran: Trump ni kijakazi cha Netanyahu

Ubalozi wa Palestina katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kukosoa vikali sera za Rais Donald Trump wa Marekani za kuunga mkono na kuukingia kifua utawala wa Kizayuni wa Israel, umebainisha kuwa Trump anapokea na kutekeleza maagizo kutoka kwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel.

Ubalozi huo wa Palestina hapa Tehran umeyasema hayo katika taarifa yake ya kulaani ukatili mpya wa utawala haramu wa Israel, dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, "Rais wa sasa wa Marekani anapokea maagizo kutoka kwa Wazayuni na Netanyahu, na (rais huyo) amekuwa akitekeleza yale yote anayoamrishwa."

Taarifa hiyo imesema mashambulizi ya ukatili ya hivi karibuni ya adui Mzayuni dhidi ya Wapalestina wasio na hatia wa Gaza yamefanyika kwa kuwa Wazayuni hawathamini maisha ya Wapalestina.

Trump na Netanyahu

Baada ya makundi ya muqawama ya Palestina kutoa kipigo na majibu makali kwa mashambulizi ya hivi karibuni ya Israel, kwa mara ya pili na katika muda wa miezi sita utawala huo khabithi ulilazimika kukubali kusitisha vita ulivyovianzisha huko Gaza. 

Kadhalika taarifa hiyo ya ubalozi wa Palestina katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekosoa vikali sera ya kiuadui ya Trump dhidi ya Mexico, Venezuela, na Korea Kaskazini ya eti kutaka 'kueleta mabadiliko ya uongozi'.