Wapalestina 304 wameshauawa shahidi tangu yalipoanza maandamano ya "Haki ya Kurejea"
(last modified Sun, 12 May 2019 02:36:44 GMT )
May 12, 2019 02:36 UTC
  • Wapalestina 304 wameshauawa shahidi tangu yalipoanza maandamano ya

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, hadi hivi sasa Wapalestina 304 wameshauawa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi makatili wa Israel wakiwemo watoto wadogo 59 na wanawake 10 tangu yalipoanza maandamano ya "Haki ya Kurejea" ya Wapaelstina tarehe 30 Machi mwaka jana 2018.

Wizara hiyo ya afya ya Palestina imesema kuwa, katika muda huo, Wapalestina 17 na 301 wamepigwa risasi na wanajeshi wa Israel, wakati Wapalestina hao wakiwa katika maandamano hayo ya amani.

Maandamano ya "Haki ya Kurejea" ya kupigania Wapalestina kurejea katika ardhi za mababu zao zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni wa Israel yalianza tarehe 30 Machi 2018 siku ambayo ilisadifiana na kumbukumbu ya "Siku ya Ardhi" huko Palestina. Maandamano hayo hufanyika kila Ijumaa katika mpaka wa Ukanda wa Ghaza na maeneo mengine ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Maandamano ya "Haki ya Kurejea" ya wananchi wa Ghaza huko Palestina

 

Siku ya Ardhi inayoadhimishwa kila mwaka huko Palestina ni kumbukumbu ya uamuzi wa utawala wa Kizayuni wa kuteka ardhi za Wapaelstina tarehe 30 Machi 1976 na kuziingiza ardhi hizo katika maeneo mengine ya Wapalestina ambayo imekuwa ikiyakalia kwa mabavu tangu mwaka 1948.

Hadi leo hii utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kuteka ardhi za Wapalestina na kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kwa lengo la kuziyahudisha ardhi hizo na kufuta kabisa utambulisho wake wa Kiislamu-Kipalestina.

Tags