Palestina yatoa taarifa kulaani mashambulizi dhidi ya hospitali za Quds
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56483-palestina_yatoa_taarifa_kulaani_mashambulizi_dhidi_ya_hospitali_za_quds
Waziri wa Afya wa Palestina amelaani hatua ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni ya kuvamia hospitali katika mji wa Quds.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Oct 08, 2019 01:10 UTC
  • Palestina yatoa taarifa kulaani mashambulizi dhidi ya hospitali za Quds

Waziri wa Afya wa Palestina amelaani hatua ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni ya kuvamia hospitali katika mji wa Quds.

Mai al Kaila Waziri wa Afya wa Palestina alisema jana Jumatatu kuwa, mashambulizi ya silaha yaliyofanywa na wanajeshi wa Israel na mbwa wa polisi wa utawala huo katika hospitali ya al Matal'a katika mji wa Quds yanaonyesha dhulma na ukandamizaji wa Israel dhidi ya wananchi, wagonjwa na taasisi za kitiba za Palestina. Waziri wa Afya wa Palestina ameongeza kuwa, wanajeshi wa Kizayuni wanaendelea  kuzivamia hospitali katika mji wa Quds. Mai al Kaila amesisitiza kuwa hakuna mtu yoyote katika ngazi ya kimataifa anayeweza kukabiliana na jinai za utawala wa Kizayuni; na ndio maana utawala huo unaendeleza jinai zake kila uchao dhidi ya raia wa Wapalestina. 

Maji wa Quds (Jerusalem) unaokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel

Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina pia imelaani mashambulizi katika hospitali ya al Matal'a katika mji wa Quds na kuyataja kuwa ni uchokozi dhidi ya mistari yote myekundu na ni kudhalilisha thamani na utu wa mwanadamu. Wizara hiyo aidha imetangaza kuwa uvamizi huo wa kukaririwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa na haki za binadamu na kwamba kimya cha jamii ya kimataifa mbele ya jinai za Israel kinautia kiburi na kuushawishi utawala huo ghasibu kuendelea jinai zake dhidi ya raia wa Palestina.