Benki nchini Lebanon zafunguliwa chini ya ulinzi mkali baada ya ghasia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i57371-benki_nchini_lebanon_zafunguliwa_chini_ya_ulinzi_mkali_baada_ya_ghasia
Kwa mara nyingine benki za Lebanon zimefunguliwa na kuanza shughuli zake chini ya ulinzi mkali wa maafisa usalama wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 20, 2019 02:29 UTC
  • Benki nchini Lebanon zafunguliwa chini ya ulinzi mkali baada ya ghasia

Kwa mara nyingine benki za Lebanon zimefunguliwa na kuanza shughuli zake chini ya ulinzi mkali wa maafisa usalama wa nchi hiyo.

Kufunguliwa benki hizo ambazo zilipigwa kufuli tangu kulipoibuka ghasia, kumejiri chini ya usimamizi wa karibu maafisa usalama 1600 ambao wamepewa jukumu la kutoa ulinzi kwa benki hizo na wafanyakazi wake kutokana na aina yoyote ya hujuma tarajiwa dhidi yao. Aidha hatua hiyo imefanyika katika hali ambayo benki zilikuwa zimeainisha viwango vya kuchukua fedha za malimbikizo, kwa utaratibu kwamba kila wiki mtu anaweza kuchukua kiasi cha dola 1000 pekee katika malimbikizo hayo.

Elie Ferzli, Naibu Spika wa Bunge la Lebanon

Kwa upande wake Elie Ferzli, Naibu Spika wa Bunge la Lebanon pia ameelezea kufunguliwa bunge la nchi hiyo ikiwa ni baada ya kupita siku 33 za kufungwa kwake. Inafaa kuashiria kuwa, Lebanon ilikumbwa na ghasia za maandamano ya wananchi kuanzia tarehe 17 Oktoba mwaka huu. Moja ya sababu kuu za kuibuka maandamano hayo, ni mgogoro wa kiuchumi pamoja na ufisadi mkubwa uliotawala katika ngazi tofauti za nchi hiyo ya Kiarabu, hususan katika uga wa masuala ya kifedha.