Uturuki yatuma zana mpya za kijeshi mkoani Idlib, Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i59679-uturuki_yatuma_zana_mpya_za_kijeshi_mkoani_idlib_syria
Duru za habari zimeripoti kwamba jeshi la Uturuki limetuma kwa mara nyingine zana mpya za kijeshi kwenda viunga vya mji wa Idlib, nchini Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 11, 2020 07:44 UTC
  • Uturuki yatuma zana mpya za kijeshi mkoani Idlib, Syria

Duru za habari zimeripoti kwamba jeshi la Uturuki limetuma kwa mara nyingine zana mpya za kijeshi kwenda viunga vya mji wa Idlib, nchini Syria.

Televisheni ya Sky News imeripoti kwamba, msafara mpya wa kijeshi wa Uturuki umeingia Idlib kupitia kivuko cha Kafr Lusin. Hii ni katika hali ambayo hivi karibuni marais wa Uturuki na Russia walikutana mjini Moscow na kufikia makubaliano ya usitishaji vita huko Idlib. Ni zaidi ya miezi miwili sasa ambapo jeshi la Syria lilianzisha operesheni ya kuusafisha mji wa Idlib kutokana na magaidi, hata hivyo Uturuki ambayo inapinga vikali upoeresheni hiyo na kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, imevamia na kuzikalia kwa mabavu ardhi za nchi hiyo ya Kiarabu na hivyo kuibua vita kati ya pande mbili.

Uvamizi wa jeshi la Uturuki katika ardhi za Syria, kwa lengo la kuwaunga mkono magaidi

Katika uwanja huo hivi karibuni Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki alikiri juu ya hasara za kiroho na mali za jeshi la nchi yake huko Idlib, kaskazini magharibi mwa Syria kufuatia mapigano makali kati ya askari wa nchi mbili. Kwa mujibu wa rais huyo, katika mapigano hayo, serikali ya Ankara ilipata hasara kubwa ambayo inafikia mamia ya askari.