Harakati za mapambano Palestina zapongeza hatua ya Ansarullah huko Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i60008-harakati_za_mapambano_palestina_zapongeza_hatua_ya_ansarullah_huko_yemen
Makundi na harakati za mapambano ya ukombozi huko Palestina zimepongeza sana pendekezo lililotolewa na harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah kuhusu suala la kubadilishana mateka wa Saudi Arabia na Wapalestina wanaoshikiliwa nchini Saudia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 27, 2020 20:35 UTC
  • Harakati za mapambano Palestina zapongeza hatua ya Ansarullah huko Yemen

Makundi na harakati za mapambano ya ukombozi huko Palestina zimepongeza sana pendekezo lililotolewa na harakati ya wananchi wa Yemen ya Ansarullah kuhusu suala la kubadilishana mateka wa Saudi Arabia na Wapalestina wanaoshikiliwa nchini Saudia.

Mjumbe wa ngazi za juu wa Harakkati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas), Mahmoud al Zahhar amesema kuwa, Wapalestina hao wamekuwa wakiishi nchini Saudi Arabia kwa miaka mingi na kwamba uamuzi wa wanapambano wa Yemen unalenga kuachiwa huru Wapalestina hao wanaoshikiliwa katika jela za Saudia. 

Taarifa iliyotolewa na Hamas imesema inapongeza hatua hiyo inayoakisi mshikamano na udugu wa Wayemeni na Waislamu wenzao wa Palestina na kwamba ni uungaji mkono mkubwa kwa mapambano na kusimama imara kwa taifa hilo.

Hamas pia imeutaka utawala wa kifalme wa Saudi Arabia kuwaachia huru Wapalestina wote wanaoshikiliwa katika jela za nchi hiyo hussan Dokta Muhammad al Khidhri Abu Halah.

Hamas imesema Wapalestina hao wanashikiliwa katika jela za Saudi Arabia bila ya kosa lolote.

Abdul Malik al Houthi

Itakumbukwa kuwa kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, Abdul Malik al Houthi Alkhamisi ilitoa hotuba kwa mnasaba wa kutimia miaka mitano tangu Saudi Arabia ianzishe vita dhidi ya taifa la Yemen mwezi Machi mwaka 2015 na akasema, harakati hiyo iko tayari kuwaachia huru rubani mmoja na maafisa wanne wa Saudia mkabala wa utawala huo kuwaachia huru wanaharakati wa Hamas wanaoshikiliwa katika jela za Sudi Arabia.

Harakati ya Ukombozi wa Palestina pia imetoa taarifa ikisema pendekezo hilo la Ansarullah linaakisi misimamo ya siku zote na asili ya taifa la Yemen ya kuwatetea Wapalestina na mapambano yao dhidi ya Wazayuni maghasibu.

Mapema jana msemaji wa Hamas, Sami Abu Zuhri alisema kuwa Saudi Arabia inawashikilia jela Wapalestina 60 na kwamba baadhi yao ni wajumbe wa harakati hiyo au waungaji mkono wake ambao wanaishi nchini humo kwa zaidi ya miaka 30.