Vita vya maneno vyashtadi kati ya Imarati na Uturuki
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i60724-vita_vya_maneno_vyashtadi_kati_ya_imarati_na_uturuki
Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imeitaka Imarati kukomesha misimamo yake ya uhasama dhidi ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 01, 2020 21:06 UTC
  • Vita vya maneno vyashtadi kati ya Imarati na Uturuki

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imeitaka Imarati kukomesha misimamo yake ya uhasama dhidi ya nchi hiyo.

Hami Aksoy, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki amesema kuwa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Imarati ni njama ya kufunika ukweli wa siasa za unafiki za nchi hiyo ambayo inawaunga mkono kwa hali na mali wafanya mapinduzi ya kijeshi (yaani wapiganaji wa Khalifa Haftar nchini Libya.) Amesisitiza kwamba Uturuki inaheshimu umoja wa kisiasa wa nchi za Kiarabu ikiwemo Libya na pia umoja wa ardhi za nchi nyingine. Alkhamisi iliyopita Wizara ya Mambo ya Nje ya Imarati sambamba na kusisitizia msimamo wake wa kuunga mkono njia ya utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Libya kupitia kongamano la Berlin, Ujerumani, pia ilionyesha wasi wasi wake kuhusu uingiliaji wa Uturuki katika masuala ya ndani ya nchi za Kiarabu hususan Libya.

Hami Aksoy, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki

Hami Aksoy, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ameashiria uingiliaji wa Imarati nchini Yemen, Syria na nchi za Pembe ya Afrika na kusema kuwa, jamii ya kimataifa iko macho na hatua mbaya za Imarati zenye lengo la kuibua ghasia na kuchafua usalama katika kila eneo lenye amani kimataifa, na kuwa uingiliaji wa Imarati hauishii tu nchini Libya.